Na Abel Paul, Jeshi la Polisi-Arusha
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani kwa pamoja wamesema serikali itaendelea Kusimamia Usalama wa vyombo vya moto hapa nchini na kufanya kaguzi za mara kwa mara pamoja na kutoa elimu kwa madereva ili kumaliza ajali nchini huku mamlaka hiyo ikiwataka mawakala wa mabasi kuandika taarifaa kikamilifu ili kuwapa haki abiria kipindi inapotokea swala la malipo ama ajali.
Hayo yamesemwa Mapema leo Disemba 24,2023 katika kituo kikuu cha mabasi Jijini Arusha na Bw. Johansen Kahatano, Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa Barabara kutoka makao makuu LATRA ambapo amebainisha kuwa wapo katika muendelezo wa ukaguzi wa vyombo vya moto na kufuatilia huduma za usafirishaji ili kubaini changamoto zilizopo na kuondoa changamoto zilizopo.
Ameongeza kuwa katika ukaguzi huo wameangalia nauli zinazolipwa kama ni halali zillizotolewa na serikali mapema mwezi huu huku akiwapongeza watoa huduma kwa kujipanga vyema kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kwa kutoa huduma nzuri kwa wananchi ambapo amesema kuwa kuna changamoto ndogo zilizopo ni uandishi wa taarifa za abiria ambazo ni muhimu katika matumizi ya malipo ya kifedha na huduma pindi tatizo linapotokea ambapo amewataka mawakala kurekebisha mara moja changamoto hiyo.
Aidha Bwana Kahatano amesisistiza kuwa mawakala kote nchini wanapaswa kufuata sheria zilizopo huku akiwataka kuandika taarifa kamili za abiri ambazo zipo kwa mujibu wa sheria nataratibu za mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini LATRA,Pia amewataka mawakala hao kuandika vyema utambulisho wa mizigo ya abiri ili kuondoa changamoto ya upotevu wa mizigo ya abiria.
Nao baadhi ya abiria wanaotumia vyombo hivyo Kwenda maeneo tofauti tofauti ya nchi wasema ni vyema abiria wakatekeleza wajibu wao pindi wanaponda magari hayo kufunga mikanda ili iwasadie huku wakitaka madereva nao kufuata sheria za usalama barabarani zilizopo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa madereva Arusha,Moshi katika kituo kikuu cha mabasi jijini Arusha Bwana Joseph Mwacha asema kwa upande wao madereva wa Mkoa huo wamekubaliana kufanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa ili kuondokana ajali huku akiipongeza LATRA na Jeshi la Polisi kikosi cha usalama Barabarani kwa kuongeza askari ambao wamedhibiti vitendo vya uhalifu katika kituo hicho.