Mhandisi Leonard Qoqona akizungumza baada ya Makabidhiano ya Eneo la kujenga Tangi la Maji litakalokua na Ujazo wa Liter Milioni Moja litakalo sambaza Maji katika Eneo la Viwanda Dunga Zuze Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwananchi wa Dunga Zuze akitoa shukrani baada ya kufanyika kwa Makabidhiano ya Eneo la kujenga Tangi la Maji litakalokua na Ujazo wa Liter Milioni litakalo sambaza Maji katika Eneo la Viwanda Dunga Zuze Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Katibu Mkuu Wiazra ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Ali Khamis Juma akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya Makabidhiano ya Eneo la kujenga Tangi la Maji litakalokua na Ujazo wa Liter Milioni Moja litakalo sambaza Maji katika Eneo la Viwanda Dunga Zuze Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Eneo ambalo litatumika kwa ajili ya kujengwa kwa Tangi la Maji litakalokua na Ujazo wa Liter Milioni Moja litakalo sambaza Maji katika Eneo la Viwanda Dunga Zuze Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
………….
Na Ali Issa Maelezo 20/12/2023.
Zaidi ya shilingi bilioni tatu zitatumika katika ujenzi wa miundo mbinu ya maji katika Eneo la Viwanda Dunga Zuze.
Hayo yamesemwa leo huko Dunga Zuze na Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Ali Khamis Juma wakati wa makabidhiano na Kampuni ya Simba Development kwa madhumuni ya ujenzi wa miundo mbinu ya maji ikiwemo tangi la lita milioni moja na visima vitano pamoja na usambazaji wa maji katika eneo lote la viwanda.
“Huu ni ujenzi wa tangi moja na visima vitano pamoja na usambazaji wa miundo mbinu ya maji katika eneo lote la viwanda.” alisema katibu.
Amesema mradi huo utachukua miezi minane hadi kumalizika kwake kuazia tarehe ya leo hadi Agosti 2024 mwakani.
Aidha alifahamisha kuwa ujenzi huo pia utawanufaisha wananchi wanaokaa maeneo ya karibu ambao tayari wameshalipwa fidia kwa maeneo yaliochukuliwa kwa ajili ya kupisha mradi wa ujenzi huo.
Aidha alimuuomba Mkandarasi huyo kuwafikiria wananchi wa maeneo hayo ili kuwapa kipaumbele cha kuwapatia kazi ambazo watazimudu kuzifanya.
Nae Mkandarasi Mkuu kutoka Kampuni ya Simba Development wa Nurdin Hassan ameahidi kuukamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa kutokana na uzoefu mkubwa wa ujenzi huo, sambamba na hiyo wamewahi kujenga matangi 10 ikiwemo matano Pemba na matano Unguja.
Aidha amesema atakuwa na mashirikiano na wananchi wa eneo hilo pamoja na kuwapatia kazi kadiri ujenzi utavyoendelea.
Nae mmoja wa wananchi hao (Mkulima) Omar Ali Haji amesema kuwa wameridhika na malipo waliyopata na kuiomba Serikali kuendelea kuwapatia maendeleo katika maeneo yao.