Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo, (katika), Akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari akitoa taarifa ya Operesheni maalum ya kukamata Dawa, Vifaa Tiba tiba na Vtendanishi Bandia, duni na zisizosajiliwa uliofanyika leo Diesemba 20, 2023 Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo, Akionesha kwa waandishi wa Habari moja ya Dawa bandia zilizokamatwa kwenye Operesheni hiyo, kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo Diesemba 20, 2023 Jijini Dar es salaam.
Msajiri wa Baraza la Famasia, Elizabeth Shekalaghe, (kushoto), akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika leo Disemba 20, 2023, Katika Ofisi za TMDA Jijini Dar es Salaam.
Naibu Kamisha wa Jeshi la Polisi, CID Daniel Nyambabe, akizungumzia ushiriki wao katika Operesheni hiyo, iliyofanyika kwenye mikoa 13 ya nchini.
………………………..
Na Sophia Kingimali
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bw. Adam Fimbo ametoa Onyo kwa watu wanaojihusisha na utengenezaji,usambazaji na uuzaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi bandia kuacha kufanya hivyo kwani ni hatari kwa afya ya jamii.
Hayo ameyasema leo Desemba 20,2023 jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya operesheni maalum ya kukamata dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya serikali vinavyuzwa kwenye maduka binafsi pamoja na vifaa, dawa Bandia,duni,zisizo na usajili na dawa za kulevya katika mkutano uliofanyika tarehe 20 mpaka 24, Novemba 2023 katika mikoa 13 nchini.
Amesema operesheni hiyo ililenga kubaini na kuchukua hatua dhidi ya makosa ya ukiukwaji wa sheria ya dawa na vifaa tiba sura ya 219 ikiwemo uwepo wa sehemu za biashara za dawa na vifaa tiba zinazoendeshwa bila kuwa na vibali kutoka mamlaka husika.
“Wilaya au mikoa husika ilichaguliwa kutokana na rekodi za matokeo ya miaka ya nyuma ya kaguzi mbalimbali za TMDA na pia taarifa za kiintelijensia kutoka katika vyombo vya udhibiti”.amesema
Ameongeza kuwa watoa huduma za afya kwenye hospitali vituo vya afya na zahanati za serikali kuacha kuiba dawa,vifaa tiba na vitendanishi na kuuza kwenye hospital na maduka binafsi kwa lengo la kujipatia kipato kisicho halali kwani hatua kali za kisheria zitachukulia kwa atakaefanya hivyo.
“Nayaelekeza mabaraza ya kitaaluma yaani mabaraza la famasia na lile la mifugo kufanya ukaguzi ili kuangalia kama wataalam wanapaswa kusimamia maduka hayo”amesema
Kwa upande wake msajiri wa baraza la phamasia bi Elizabeth Shekalage amewataka wataalam wote wa afya watumie weledi katika katika kununua dawa ili kulinda afya za wananchi.
Aidha Bi Elizabeth amewataka pia kutoa taarifa katika maeneo yao lakini pia kutumia mfumo rasmi wa ununuzi wa dawa na kuacha kununua dawa mikononi.
“Wamiliki wote wa maduka ya dawa wanapaswa kununua dawa katika mfumo rasmi dawa zilizosajiliwa lazima zipite kwenye mfumo rasmi hizo zinazopita mikononi ni zile ambazo hazijasajiliwa na ni hatari kwa afya ya binadamu”amesema
Katika ukaguzi huo uliohusisha mikoa 13 ikiwemo Dar es salaam,Dodoma,Morogoro,Kigoma,Katavi,Mwanza,Simiyu,Arusha,Kilimanjaro,Mbeya,Songwe,Lindi na Ruvuma ambapo jumla ya majengo 777 yalikaguliwa kati yake 283 ni famasia, 23 maduka ya vifaa tiba 9 maghala ya dawa,maghala 2 ya vifaa tiba,maduka 105 ya dawa za mifugo,272 maduka ya dawa muhimu za binadamu(DLDM)30 vituo vya kutolea huduma za afya,32 maabara na kiwanda kimoja.
Operesheni hiyo ilifanywa kwa kushirikiana na TMDA,Ofisi ya Rais mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya(DCEA)Baraza la Famasia,TAMISEMI na jeshi la polisi.