Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Msali asili na Mifugo Shamata Shaame Khamis akizungumza na Wandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio na Changamota za Wizara yake kuelekea miaka Sitini ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC Mnazi mmoja Zanizbar.
Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Msali asili na Mifugo Shamata Shaame Khamis akizungumza na Wandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio na Changamota za Wizara yake kuelekea miaka Sitini ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC Mnazi mmoja Zanizbar.
Afisa Habari kutoka Idara ya Habari Maelezo Takdiri Ali akiuliza maswali katika Mkutano wa Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Mali asili na Mifugo Shamata Shaame Khamis wakati akizungumza na Wandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio na Changamota za Wizara yake kuelekea miaka Sitini ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC Mnazi mmoja Zanizbar.
Mwandishi wa Habari kutoka ZBC Fatma Abdalla akiuliza maswali katika Mkutano wa Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Mali asili na Mifugo Shamata Shaame Khamis wakati akizungumza na Wandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio na Changamota za Wizara yake kuelekea miaka Sitini ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC Mnazi mmoja Zanizbar.
Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Msali asili na Mifugo Shamata Shaame Khamis akisisitiza jambo wakati akijibu maswali ya waandishi wa Habari alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na Mafanikio na Changamota za Wizara yake kuelekea miaka Sitini ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC Mnazi mmoja Zanizbar. (PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZNAZIBAR.19/12/2023)
……………
Na TAKDIR ALI – HABARI MAELEZO, 19/12/2023.
Sekta ya kilimo imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza pato la Taifa.
Hayo yameelezwa na Waziri wa kilimo ,Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu maadhiisho ya miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar huko katika Ukumbi wa ZBC Karume house.
Amesema kuanzia mwaka 2013 hadi 2022 mchango wa sekta ya kilimo umekuwa kwa kufikia asilimia 20.8 hadi asilimia 27.1.
Amefahamisha kuwa Serikali imekamilisha ujenzi wa ghala la kuhifadhia chakula lililopo Kizimbani Unguja lenye uwezo wa kuhifadhi tani 1,500 za nafaka.
Aidha amesema Katika jitihada za kuimarisha zao la karafuu na minazi kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2023, Serikali imefanikiwa kuotesha miche 539,316 ya mikarafuu na miche 12,340 ya minazi.
Mbali na hayo ameelezea kuwa katika kuhamasisha jamii kupunguza matumizi ya nishati ya kuni na mkaa matumizi ya nishati ya gesi imeongezeka asilimia 12.6 ya kaya za kawaida.
Hata hivyo amesema hali hiyo imetokana na jitihada za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala na udhibiti wa uharibifu wa misitu