Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga akizungumza jambo na Wahariri wa Vyombo vya habari katika kikao kazi kilichofanyika leo Desemba 18, 2023 Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa PSSSF Tower.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) Bi. Anjela Mziray akizungumza jambo na Wahariri wa Vyombo vya habari katika kikao kazi kilichofanyika leo Desemba 18, 2023 Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa PSSSF Tower.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Afisa wa Habari Mwandamizi Mkuu – Habari Maelezo, Bi. Liliani Shirima akizungumza jambo na Wahariri wa Vyombo vya habari katika kikao kazi kilichofanyika leo Desemba 18, 2023 Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa PSSSF Tower.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Jene Mihanji akizungumza jambo na Wahariri wa Vyombo vya habari katika kikao kazi kilichofanyika leo Desemba 18, 2023 Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa PSSSF Tower.
Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika kikao kazi na Menejimenti ya Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) kilichofanyika leo Desemba 18, 2023 Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa PSSSF Tower.
……….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) imejipanga kufanya maboresho ya kitita cha mafao katika maeneo tofauti ikiwemo kuongeza jumla ya dawa 124 kutoka katika orodha ya dawa muhimu ya Taifa (NEMLIT), kuondoa changamoto za uandishi wa majina ya baadhi ya vipimo pamoja na kuongeza wigo wa huduma za kibingwa za upasuaji katika hospitali zote za rufaa ya kanda na Taifa.
Imeelezwa kuwa wameweka usawa wa ada ya kumuona daktari pamoja kutambua uwepo wa kada ya madaktari katika ngazi ya afya ya msingi jambo ambalo litawasaidia watanzania kupata huduma bora kupitia mfuko huo.
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika kikao kazi kilichofanyika leo Desemba 18, 2023 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa PSSSF Tower, Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga, amesema kuwa maboresho hayo yanakwenda kuleta ahueni kwa wanachama na wadau kwa ujumla ili kuhakikisha wanatoa huduma bora.
Bw. Konga amesema kuwa maboresho yamejumuisha dawa zenye nguvu (strength) na muundo (formulation) kwa kuzingatia upatikanaji wa dawa katika soko pamoja na mabadiliko katika ngazi za matumizi ya dawa kama ilivyoanishwa mwongozo wa tiba nchini.
“Katika huduma ya upasuaji na vipimo tutafanya maboresho ambayo yamelenga kwenda sambamba na mapitio ya gharama halisi na uchambuzi wa uhalisia wa bei katika soko” amesema Bw. Konga.
Amefafanua kuwa watazingatia mambo muhimu katika maboresho hayo ikiwemo kufanya utafiti wa gharama halisi za matibabu katika soko pamoja na kushirikisha wadau wa sekta binafsi kwa lengo la kupata maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu kitita.
Amefafanua kuwa katika kuhakikisha kunakuwa na udhibiti wa matumizi wataimarisha utambuzi wa wanufaika katika vituo vya kutolea huduma kwa kutumia alama za vidole pamoja na kuweka “Platform” ya kieletroniki itakayowezesha watoa huduma kubadilisha taarifa za wagonjwa miongoni mwa vituo.
Amesema kuwa wameweka utaratibu utakaowezesha wanufaika kuzingatia utaratibu wa rufaa, kuongeza huduma zitakazo hitaji uchangiaji (co- payments) na ukomo wa ugharamiaji kwa baadhi ya huduma za makundi ya wanachama (copping).
“Kutakuwa na mfumo wa utambuzi wa madaktari katika vituo vya kutolea huduma nchini, pia tutachukua hatua stahiki kwa watakaodhibitika kujihusisha na vitendo vya udanganyifu” amesema Bw. Konga.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Afisa wa Habari Mwandamizi Mkuu – Habari Maelezo, Bi. Liliani Shirima, amesema kuwa ni jambo jema kukutana na makundi muhimu ikiwemo wahariri ambao wanajukumu la kuhabarisha umma pamoja na kutoa elimu.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Jene Mihanji, amesema kuwa vyombo vya habari vitaendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha malengo yanafikiwa.
“Tutaendelea kutoa ushirikiano ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu huduma za NHIF” amesema Bi.Mihanji.