Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Rashid Hadid Rashid akizungumzia fursa zinazopatikana katika Mkoa huo huko ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B” Unguja.
Mkurugenzi wa habari na matukio Shirika la utangazaji Zanzibar ZBC Salum Ramadhan akizungumza machache na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini unguja Rashid Hadid Rashid kuzungumzia fursa zinazopatikana katika Mkoa huo,huko ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B” Unguja.
Msaidzi mkurugenzi wakala wa uwekezaji ZIPA Saleh sani akizungumzia fursa zinazopatikana za uwekezaji katika mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa majadiliano yaliyoangazia fursa na mbinu za kuzifikia uliofanyika ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B”.
Mkurugenzi mafunzo wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi (ZEEA)Fatma Mohammed Juma akizungumzia fursa zinazopatikana za uwezeshaji wananchi kiuchumi katika mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wakati wa majadiliano yaliyoangazia fursa na mbinu za kuzifikia yaliofanyika ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B”.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa kaskazini unguja wakiwa katika hafla ya majadiliano yalioangazia fursa zinazopatikana katika mkoa huo na mbinu za kuzifikia yaliyofanyika ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B”.
Baadhi ya viongozi wa chama na Serikali pamoja na wananchi wa Mkoa wa kaskazini unguja wakifuatilia majadiliano yaliyoangazia fursa zinazopatikana katika mkoa huo na mbinu za kuzifikia huko ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B”.
Mohammed Makame Juma mkaazi wa Potoa akichangia wakati wa majadiliano yalioangazia fursa za mkoa wa kaskazini unguja na namna ya kuzifiki, huko ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B”.
Mjasiriamali kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja Fatma Saleh Ukindu akitoa ushuhuda wa kufanikiwa kupata mkopo wa INUKA kupitia ZEEA wakati wa majadiliano ya kuangazia fursa za mkoa huo na namna ya kuzifiki, huko ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B”.
Ashura Muhammed Haji kutoka baraza la vijana Kaskazini unguja akichangia wakati wa majadiliano yalioangazia fursa za mkoa wa kaskazini unguja na namna ya kuzifiki, huko ukumbi wa Mitihani Bumbwini Kaskazini “B”.
PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR
NA RAHMA KHAMIS, MAELEZO
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Rashid Hadid Rashid amewataka Vijana kuzikimbilia fursa zinazopatikana ndani ya Mkoa huo ili kujiendeleza kiuchumi.
Akizungumza wakati wa mjadala ulioangazia kuzielezea fursa za mkoa huo na namna ya kuzifikia huko ukumbi wa mitihani Bumbwini amesema fursa ni kitu muhimu kwa vijana kwani inawawezesha kujikimu katika maisha yao ya kila siku.
Amesema Mkoa wa Kaskazini una fursa nyingi ikiwemo Utalii, Kilimo, Afya na Elimu hivyo ni wajibu kwa kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika fursa hizo ili kunufaika nazo.
“Mkoa wetu umebarikiwa fursa nyingi za kuwainua wananchi hatuna budi kuzitumia fursa hizi ili kujikomboa na hali ngumu ya maisha” alissisitiza Hadid.
Aidha amefahamisha kuwa katika kuwajengea uwezo vijana, Serikali imejenga masoko saba katika maeneo mabali mbali ndani ya Mkoa huo ili kuwawezsha vijana kupata fursa za ajira hivyo ni wajibu wao kujipanga na kuzitumia fursa hizo kwa lengo la kufaidika.
Ameongeza kuwa katika kuhakikisha vijana wanazitumia fursa hizo ipasavyo zaidi ya vijana elfu moja tayari wameshapatiwa mikopo ili kujiwezesha kiuchumi.
Nae Msaidizi Mkurugenzi Mamlaka ya Uwekezaji (ZIPA) Saleh Said amesema miongoni mwa majukumu ya ZIPA ni kusajili miradi yote iliyopo katika Mkoa na kuweka viwango vya uwekezaji kwa wageni
Ameongeza kuwa katika kuwapatia fursa wawekezaji wa ndani mamlaka imeweka unafuu kwa wawekezaji wa ndani ukilinganisha na wageni ambao wahitajika kulipa zaidi ya dola millioni mbili.
Wakitoa ushauri wao wananchi wa Mkoa wa Kaskazin Unguja wamewaomba mamlaka husika kuwapatia elimu ya miradi inayojengwa pamoja na kuwekewa maafisa katika kila Wilaya ili waweze kupata mikopo kwa urahisi na kuondoa usumbufu wanapohitaji mikopo hiyo.
Majadiliano hayo ni mwendelezo wa Kampeni ya mkono kwa mkono kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.