Naibu Waziri wa kilimo ,David Silinde akizungumza katika mahafali hayo ya chuo cha uhasibu Arusha 
Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha ,Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza katika mahafali hayo .
Wahitimu wa chuo cha uhasibu Arusha wakimsikiliza mgeni rasmi katika mahafali hayo.
Julieth Laizer ,Arusha .
Serikali imekipongeza chuo cha Uhasibu Arusha kwa kuja na mabadiliko ya mitaala ya elimu katika upande wa kilimo, Biashara ,ufundi,utalii ambayo kwa kiasi kikubwa inayoakisi  mazingira halisi ya  kuisaidia Tanzania katika ukukuzaji wa uchumi.
Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde ameyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa fedha  wakati akizungumza katika  mahafali ya 25 ya  Chuo  cha Uhasibu Arusha yenye wahitimu 5387 yaliyofanyika Katika hoteli ya Ngurdoto wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Amesema serikali imewekeza fedha nyingi katika vyuo vya elimu ya kati na vyuo vikuu, kutokana na jitihada kubwa  zinazofanywa na  Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watanzania wanapata elimu bora na yenye usawa.
“Niseme chuo kimeona mbali  kwa kuanzisha mitaala yenye kukidhi huhitaji, na kuwa mstari wa mbele katika kuongeza idadi ya wanafunzi,kuanzisha mitaala  na fani zinazojibu changamoto kwa Taifa hili, ninawapongeza sana kwa mpango huu ” amesema .
Silinde ametoa  rai kwa Taasisi  ya elimu za juu kufanya tafiti  na kuanzisha mitaala itakayotoa majawabu na kujibu changamoto zinazolikabili  Taifa , ili wahitimu hao waliopata elimu wakalete matokeo chanya ya  utekelezaji wa malengo ya millennia”amesema Silinde .
“Nafahamu kila mmoja amefanya tafiti kama takwa la chuo kabla ya kuhitimu, ni imani yangu kila mhitimu aishirikishe jamii yake ,na kutokufungia matokeo hayo kabatini, tumieni  utafiti mlioufanya ili  kuongeza tija katika mabadiliko yakiuchumi.”amesema .
Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha (IAA)  Profesa Eliamani Sedoyeka amesema  chuo icho kwa sasa kina jumla ya kozi 71 ambapo 16 stashahada, 17 stashahada, uzamili 14,shahada 24 .
Ameeleza chuo kimeanzisha shahada mpya ya medua bainowai na mawasiliano ya umma, kutokana na mazingira ya Sasa kupitia  msisisitizo wa serikali  katika sekta ya  elimu  yakutengeneza kada ya viongozi katika eneo hilo katika usimamizi wa shule na maafisa elimu ngazi ya wilaya .
“Serikali iliwapatia chuo hiki shilingi   48 bilioni  na mipango ni kukakikisha chuo kinatoa  misingi ya weledi na umahiri  na kuwa kinara  katika maeneo yote , huku mipango mikakati ya miaka 5 ni  kuongeza wigo wa kujenga miundombinu ya kufundishia,kituo cha tehama, kumbi pacha  za kufundishia katika kampasi 4 ya  Arusha,Babati, Dar es salaam, Dodoma na tuna mpango wa kuanzisha kampasi nyingine mpya ya  Songea ambapo  tayari tumepatiwa shilingi  22 bilioni na serikali kwa ajili ya kujengwa kampasi hiyo ili kutengeneza soko lenye uhakika.”amesema.
Hata hivyo ili kuhakikisha usalama wa Raia na mali zao zinalindwa  wameimarisha mahusiano  na chuo cha polisi Moshi kwa kuja na kozi  mbalimbali kwa lengo la kuvifikia vyombo vya ulinzi na usalama.
Makamu Mwenyekiti wa baraza la uongozi wa chuo hicho CPA Joseph Mwigune amesema  mahafali hayo ya 25  ni dhihirisho la jitihada na mchango mkubwa kutoka kwa  menejimenti ya Chuo kwa kusimamia majukumu yao ipasavyo ,kiutendaji nakuwezesha kupata ongezeko la wanafunzi .
Ameongeza kuwa, chuo kimekuwa  na mipango mikakati ya muda mrefu,na mfupi  waliyojiwekea ya kutoa mafunzo,utafi na ushauri wa kitaalamu katika  kuendana na Sayansi na teknolojia katika kulinda Taswira na  hadhi ya Chuo icho kwa wakati wa Sasa na ujao.