*Awezesha upatikanaji wa zaidi ya Tsh Milioni 30.
*Awezesha upatikanaji wa Mifuko 18 ya Saruji
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Ndugu Jokate Mwegelo, ameongoza Harambee ya kuchangia mwendelezo wa ujenzi wa Kanisa Katoliki Kigango cha kijiji cha Tanga Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma.
Zoezi hilo limefanyika leo tarehe 15 Disemba, 2023 aliposhiriki katika misa takatifu iliyosalishwa na Mhashamu Baba Askofu John. C. Ndimbo, Askofu Jimbo Katoliki Mbinga ya kutoa shukrani kama familia kwa nafasi ya kuaminiwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuteuliwa katika nafasi ya Katibu Mkuu wa UWT Taifa.
Katika kuchangia Ujenzi huo, Katibu Mkuu Jokate amechangia kiasi cha Tsh Milioni 5 fedha taslimu na kutoa ahadi ya kuongezea Tsh Milioni 10.
Pia, Katibu Mkuu Jokate mara baada ya kutoa salamu za shukrani, ameongoza zoezi la Harambee ambapo amewezesha kupatikana kwa fedha Tsh taslimu Tsh laki 9 na Ahadi za Jumla ya Tsh Milioni 30.
Aidha, ametoa salamu za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wana Mbinga ambapo amesema ” *Kipekee napenda kuwapa salamu za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amenituma niwaambie kuwa anawapenda, anawathamini na kuendelea kuwatumikia kuhakikisha huduma za kimaendeleo zinaendelea kufukishwa na Serikali anayoiongoza ya awamu ya sita na kuwataka nanyi muendelee kuwa na Imani naye.