NA HERI SHAABAN (ILALA)
MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema wanawake wa umoja wa wanawake UWT Wilaya ya Ilala wana jukumu la kuunda na kuwa karibu na makundi mbalimbali ya kijamii na fursa za kiuchumi kwa ajili ya kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo, alisema hayo katika semina kwa Wajumbe wa Baraza la UWT wilaya ya Ilala katika ukumbi wa mikutano Arnatoglou wilayani Ilala ambapo alisema makundi hayo yatawasaidia kuona fursa za kiuchumi ,masoko, mikopo na kupinga vitendo vya ukatili vya aina yoyote katika jinsia
“Kazi ya Umoja wanawake UWT jukumu lenu kuunda na kuwa karibu na makundi mbalimbali ya kijamii kwa ajili ya kutafuta fursa za kiuchumi za masoko ,mikopo na kupinga ukatili wa kijinsia wa aina yoyote “alisema Mpogolo.
Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo alisema hizo ndio kazi anazotakiwa kufanya mwanamke wa UWT zitakazo mfanya kuwa karibu na wananchi wapiga kura kutatua changamoto na kufatilia manyanyaso wanayofanyiwa wananchi hususani wanawake.
Aliwataka wanawake wa UWT wilaya ya Ilala kuwa wamoja na kujenga mshikamano katika kuakikisha chama cha Mapinduzi kina shika dola katika chaguzi zake zote za Serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka 2025.
Wakati huohuo akizungumzia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeanza kufanya vizuri kwenye makusanyo kwa kuongeza zaidi ya Bilioni 2.5 kwa mwezi ukilinganisha na huko nyuma ambapo sasa wanaweza fikia bilioni 8 hadi 10 kwa mwezi ukilinganisha na bilioni 5 hadi 6 huko nyuma.
Mpogolo alisema makusanyo hayo yameifanya Jiji kutengeneza Madawati 20,000 kwa shule za msingi na Viti na Meza 17,600 kwa shule za Sekondari. Hii itafanya watoto wote kukaa kwenye Viti na madawati .
Katika hatua nyingine amekemea Mgambo wa Halmashauri waache kunyanyasa wananchi na kudhurumu Mali za wafanyabishara katika halmashauri hiyo ya jiji la Dar es Salaam.
Aliwataka wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi za uchumi na za kijamii wana haki ya kuchukua fomu na kugombea nafasi yoyote.