Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw Elijah Mwandumbya (katikati), akiwa katika maandamano wakati wa Mahafali ya 21 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw Elijah Mwandumbya, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), akizungumza wakati akihutubia hadhira wakati wa hafla ya Mahafali ya 21 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa kada mbalimbali wakiwa katika hafla ya Mahafali ya 21 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw Elijah Mwandumbya, akimpongeza Mhitimu baada ya kuwatunuku shahada wahitimu wa Chuo Cha Uhasibu Tanzania (TIA) katika hafla ya Mahafali ya 21 ya Chuo hicho, yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw Elijah Mwandumbya, akimpongeza Mhitimu baada ya kutunuku shahada wahitimu wa Chuo Cha Uhasibu Tanzania (TIA) katika hafla ya Mahafali ya 21 ya Chuo hicho, yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw Elijah Mwandumbya (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chuo Cha Uhasibu Tanzania (TIA) wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William Pallangyo (wa pili kulia), baada ya hafla ya Mahafali ya 21 ya Chuo hicho, yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw Elijah Mwandumbya, akiagana na viongozi mbalimbali baada ya kuhudhuria Mahafali ya 21 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam).
………..
Na Scola Malinga, WF, Dar es Salaam
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), ameitaka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha miundombinu iliyopo inatumika kuhakikisha kampasi zote saba zinapata wanafunzi.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha, katika Mahafali ya 21 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw Elijah Mwandumbya, ameitaka Taasisi ya TIA kuweka mikakati ya kuhakikisha taarifa zinawafikia watanzania wote popote walipo ndani na nje ya nchi ili watumie fursa za kujiendeleza kielimu kupitia kozi mbalimbali, zinazotolewa kwenye Chuo.
Alisema kuwa Serikali imetumia gharama kubwa kujenga miundombinu hiyo, ikilenga kupunguza adha wakati wa uendeshaji wa shughuli za Taasisi na kuboresha utendaji na utoaji wa huduma kwa ujumla hasa katika kutoa elimu.
“Serikali inatumia fedha za watanzania kugharamia ujenzi wa miundombinu. Hakikisheni watanzania wanapata taarifa za utekelezaji wa miradi hiyo kila mara, pamoja na masuala mbalimbali yanayofanywa na Serikali kupitia Taasisi hii” alisema Bw. Mwandumbya.
Aliagiza kuwa miundombinu iliyojengwa iwekewe mikakati ya utunzaji ili idumu kwa kipindi kirefu huku ikibaki katika hali ya ubora wa kutoa elimu kwa watanzania wote.
Aidha aliwataka wafanye kazi kwa bidii, uadilifu, ubunifu, umakini, weledi na kujiepusha na uzembe, huku wakifanya kazi kwa kuzingatia Sera, Sheria, Taratibu na Kanuni ili kujiimarisha zaidi na kuweza kushindana katika soko la ajira.
“Lazima muendelee kujielimisha kwa lengo la kujenga ujuzi na maarifa ya kutosha, kadri inavyowezekana, ili muweze kutumikia taifa kwa viwango vya hali ya juu” alisema Bw. Mwandumbya.
Alifafanua kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na TIA kuhakikisha kuwa wanaweza kukabiliana na changamoto mbalimbali hasa zinazotokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia,pamoja na ongezeko la idadi ya wanachuo.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Prof. William Pallangyo, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya kusomea na kufundishia, katika kampasi za TIA kupitia Wizara ya Fedha.
Katika mahafali hayo wahitimu 7,222 wa kampasi ya Dar es Salaam, wakiwemo Wanawake 3,957 na Wanaume 3,269 walitunukiwa vyeti vya shahada mbalimbali.
Hata hivyo Wahitimu kwa kampasi zote sita ni 13,265, wakiwemo wanawake 7,155 na wanaume 6,110 isipokuwa kampasi ya saba ya Zanzibar ambayo imeanza kupokea wanafunzi mwaka huu.