OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amekemea ubabaishaji katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi Kagera.
Pia amesema yeyote atakayeingiza mikono yake wakati wa utekelezaji mradi huo atachukuliwa hatua bila kujali ni mwanasiasa au wa Serikali.
Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa kukagua eneo litakalotumika kujenga stendi ya kisasa Kykailabwa manispaa ya Bukoba.
Amesema kazi hii itasimamiwa na TARURA ambao wanakuwa chini ya Mkoa, hatutaki ubabaishaji tunataka miradi itekelezwe na yeyote atakayeingiza mkono bila kujali ni mwanasiasa au serikali nadhani nimeeleweka.”
“Kazi ifanyike vizuri ili kila mwana Kagera aliyopo ndani na je ya nchi warudi hapa wajionee matunda ya kazi iliyofanywa.”
Amesema maelekezo ya Rais Samia ni kutaka stendi ya Kagera iwe ye mfano na kusisitiza kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI itakuwa ikifanya ukaguzi wa mara kwa mara.
“Baada ya kukagua alisema baada tu upembuzi yakinifu (feasibility study) kufanyika kwenye stendi ya mabasi ya Kyakailabwa, ripoti iwasilishwe Wizarani kwa mapitio na maoni ndipo usanifu wa kina (detailed design) ufuate, tunataka stendi ya Kagera iwe ya mfano na ndio maelekezo ya Rais.”
“Usimamizi kama tulivyokubaliana TARURA watafanya usimamizi lakini wanapokuwa mikoani Tarura wanakuwa chini ya Mkoa hatutaki ubabaishaji tunataka miradi itekelezeke kikamilifu.”
Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Bukoba, Amid Njovu alisema eneo hilo lina kubwa wa ekari 14 la litakuwa na Eneo la daladala, magari binafsi na mabasi ya yaendayo mikoani.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa alisema kilio cha stendi na soko kwa wanaKagera ni cha miaka 40 na kushukuru Rais Samia Suluhu Hassan katika kutimiza hilo.”