Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete akizungumza Jijini Arusha wakati akifunga kongamano la 14 la mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi .
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete akikabidhiwa tuzo na Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB,Godfred B. Mbanyi, mara baada ya kufunga kongamano la 14 la mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi uliofanyika Jijini Arusha.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalam wa ununuzi na ugavi mara baada ya kufunga kongamano la 14 la mwaka la wa ununuzi na ugavi uliofanyika Jijini Arusha
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watendaji mara baada ya kuwasili kufunga kongamano la 14 la mwaka la wa ununuzi na ugavi uliofanyika Jijini Arusha
Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB,Godfred B. Mbanyi, akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete kwa ajili ya kufunga kongamano la 14 la mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi uliofanyika Jijini Arusha.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete akiangali tuzo aliyokabidhiwa na na Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB,Godfred B. Mbanyi, mara baada ya kufunga kongamano la 14 la mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi uliofanyika Jijini Arusha.
……….
Na Lusungu Helela – Arusha
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete anesema eneo la ununuzi wa umma limekuwa likiripotiwa kugubikwa na vitendo vya rushwa na ubadhirifu ambapo zaidi ya asilimia 72 ya bajeti ya Serikali imekuwa ikitumika kwenye manunuzi hayo ya umma
Amesema kutokana na uzito huo Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao imeamua kusanifu, kujenga na kusanikisha Mfumo wa Kitaifa wa Kielektroniki wa Ununuzi Tanzania {National e-Procurement System of Tanzania (NeST)} ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo.
Mhe.Kikwete ametoa kauli hiyo leo Jijini Arush wakati akifunga kongamano la 14 la mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi zaidi ya 900 lenye kauli mbiu “Mabadiliko ya kidijitali kwa ajili ya kuboresha usimamizi na ugavi kelekea maendeleo endelevu”
Amesema mfumo huo utasaidia kuondoa mianya ya rushwa na upendeleo na hivyo thamani ya pesa za Serikali katika bidhaa na huduma italindwa kwani kutakuwa hakuna ulazima wa watu kukutana ana kwa ana
” Ni furaha yangu mimi kama Naibu Waziri ninayeshughulikia Utawala Bora ambapo ninasimamia uzuiaji na mapambano dhidi ya Rushwa, naamini mfumo huu utaondoa hisia hasi zilizojengeka katika jamii kwenye suala la manunuzi ya umma na hivyo kuongeza uwazi ” amesema Mhe.Kikwete
Mhe.Kikwete amesema u mfumo huo utaongeza ufanisi, uwazi na ushindani katika ununuzi wa umma.
Katika hatua nyingine, Mhe.Kikwete amesema serikali haitamvumilia mtu yeyote atakayesababisha upotevu wa rasilimali za nchi huku akiwataka wasithubutu kucheza na mfumo huo mpya wa manunuzi kwa umma.
Aidha, ametoq wito kwa waajiri wote kuhakikisha wataalam wenu wamesajiliwa na wanazo sifa za kufanya kazi za ununuzi na ugavi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kupitia mfumo.