Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza katika Mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es yaliyofanyika leo Desemba 14, 2023 katika Ukumbi wa Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Makamu Mkuu Chuo Kikuu Mzumbe Profesa William Mwegoha akizungumza katika Mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es yaliyofanyika leo Desemba 14, 2023 katikaUkumbi wa Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Saida Yahya-Othman akizungumza katika Mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es yaliyofanyika leo Desemba 14, 2023 katika Ukumbi wa Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam Prof. Cyriacus Binamungu (kulia) akipokea cheti cha pongezi cha mwanataaluma kutoka kwa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein katika Mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es yaliyofanyika leo Desemba 14, 2023 katika Ukumbi wa Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Baaadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam waliofanya vizuri katika masomo yao wakipokea zawadi kutoka kwa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein katika Mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es yaliyofanyika leo Desemba 14, 2023 katika Ukumbi wa Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa ngazi mbalimbali, Wahadhiri wakiwa Mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es yaliyofanyika leo Desemba 14, 2023 katika Ukumbi wa Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.(Picha na Noel Rukanuga)
………..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wametakiwa kuwa wazalendo, kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa pamoja na kutumia maarifa na ujuzi waliopata kwa kuleta maendeleo katika jamii.
Wito huo umetolewa leo Desemba 14, 2023 na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein wakati wa Mahafali ya 22 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Dkt. Mohamed Shein amesema kuwa kujiamini, kufanya kazi kwa bidii ni njia pekee itakayowafanya wahitimu kuaminiwa katika maeneo mbalimbali katika utekelezaji wa mujukumu.
“Wahitimu mnapaswa kujikita katika kufanya tafiti ili kusaidia jamii, kuangalia mslahi ya watu, chuo katika utekelezaji wa majukumu yenu, pia tujiunge mtaandao wa Chuo ili tuweze kukisaidia chuo chetu.” amesema Mhe. Dkt. Mohamed Shein.
Aidha Mhe. Dkt. Mohamed Shein amewapongeza watumishi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na kuongeza ufanisi katika utendaji.
Amesema kuwa wakati umefika wa kuongeza kasi katika utendaji wa majukumu ili vijana waweze kupata maarifa ambayo yatawasaidia katika kufikia ndoto zao pamoja na kutatua matatizo katika jamii.
Mhe. Dkt. Mohamed Shein amewakumbusha menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kutumia fursa katika Mkoa huo ikiwemo kuendeleza ya ardhi ya Chuo ili kuongeza mapato.
“Tujenge ukumbi ambao unaweza kukidhi mahitaji chuo jambo ambalo lisaidia kuongeza mapato ya serikali” amesema Mhe. Dkt. Mohamed Shein.
Kaimu Makamu Mkuu Chuo Kikuu Mzumbe Profesa William Mwegoha, amesema kuwa wanaendelea kufanya kazi kwa uweledi mkubwa ili kufikia malengo ya chuo.
Amesema kuwa chuo kinatekeleza miradi 17 ya utafiti katika nyanja mbalimbali pamoja na kuchapisha majalada ndani na nje ya nchini.
“Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kimekuwa na utamaduni
kutoa huduma za kijamii bure ikiwemo kununua kadi 35 za bima ya afya kwa watoto katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili”amesema Profesa Mwegoha.
Amesema kuwa ili kuongeza ufanisi wamekuwa na programu ya kuwajengea uwezo wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini.
Profesa Mwegoha amewataka wahitimu
554 wa ngazi mbalimbali Ndaki ya Dar es Salaam kuwa wabunifu pamoja na kujiendeleza kitaaluma.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Saida Yahya-Othman amesema kuwa amewakumbusha wahitimu umuhimu kuongeza maarifa utafiti, uchambuzi wa mambo mbalimbali bila kuumbishwa na mtu yoyote.
Profesa Othuman amewataka kwenda kuishi kwa kuzingatia hali ya kipato halisi katika maisha pamoja na kutetea na kukosea inapobidi katika jamii.
“Tukaishi kwa kipato halali bila kufanya uharibifu wowote katika maisha na utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku kazi” amesema Profesa Othuman.
Amesema kuwa ukuaji wa teknolojia ya akili bandia umeleta changamoto katika soko la ajira, hivyo nendeni katika jamii kwani tumejifunza kwa maendeleo ya watu.
Akizungumza kwa niaba ya wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Bw. Jonathan Baraka, ametoa shukrani kwa menejimenti na wote walichangia katika safari ya kufanikisha ndoto ya kuongeza elimu katika Chuo Kikuu Mzumbe.
“Wahitimu wa shahada ya awali Ndaki ya Dar es Salaam, Tegeta tunatoa shukrani kwa msaada wenu ambao umeleta ufanisi na tija katika kipindi chote, haikuwa kazi raisi, hivyo tunawapongeza” amesema Bw. Baraka.
Bw. Baraka ametoa wito kwa wanafunzi wanaendelea na masomo kuwa na ushirikiano wa kutafuta ushauri wa wataalamu katika fani wanazosoma.
Chuo Kikuu Mzumbe : Tujifunze kwa Maendeleo ya Watu.