Na Mwandishi wetu,jeshi la Polisi- Dodoma.
Jeshi la Polisi nchini limetoa tahadhari kwa wananchi juu ya mvua zinazoendela kunyesha huku liesema linao wajibu wa kulinda maisha ya watu na mali zao, ambapo limetoa tahadhari kwa Wananchi wote kuhusiana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa Nchini.
Akitoa taarifa hiyo leo disemba 10,2023 Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema Jeshi hilo tayari limepokea taarifa mbalimbali za watu wazima na watoto kufa maji wakati wakijaribu kuvuka mito na barabara zilizojaa maji, na wengine wakiogelea kwenye mashimo, madibwi Pamoja na mabwawa yaliyojaa maji ya mvua na kusabisha vifo kwa baadhia yao.
SACP Misime amewataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa wanapotaka kuvuka mito,madaraja,makorongo ambayo yamejazwa na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo ameongeza kuwa mvua zinazoendelea kunyesha hazina urafiki na yeyote anayetakakushindana nazo.
Aidha amewaomba wazazi na walezi kuongeza ungalizi Mkubwa kwa watoto kipindi hiki cha mvua ambazo zimetabiriwa kuendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya nchi ambapo amewataka wazazi kuwaonya na kutowaruhusu kwenda kucheza au kuogelea kwenye mito,makorongo yanayopitasha maji ya mvua Pamoja na madimbwi mabwawa.
Sambamba na hilo amewasihi wananchi wote ambao wamechimba mashimo na kuyaacha wazi wayafukie ili yasihatarishe Maisha ya watu.
Msemaji wa Jeshi hilo Pia ametoa wito kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa kuendelea kushirikiana na Polisi Kata, kutoa elimu na tahadhari kwa wananchi ili kuwaepusha madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha.