Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) Bw. Erasto Simon akizungumza leo Jijini Dar es Salaam na Jukwaa la Wahariri Tanzania katika mkutano ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina uliofanyika Leo Desemba 11,2023.
Bw. Sabato Kosuri Afisa Mawasiliano Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina akifafanua baadhi ya Mambo katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam Leo Desemba 11, 2023.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) Bw. Erasto Simon akijadiliana jambo na Bw. Sabato Kosuri Afisa Mawasiliano Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam Leo Desemba 11, 2023.
Imma Mbuguni Mhariri Mtemdaji wa Gazeti la Majira akuliza swali katika mkutano huo ili kupata ufafanuzi wa naadhi ya mambo.
Jesse Kwayu kutoka Media Brain naye akauliza maswali yake uli kupata uelewa katika baadhi ya mambo yanayofanywa na wakala wa Uagizaji Mafuta wa Pamoja PBPA.
……………………….
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Mfumo wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja umeleta manufaa makubwa nchini kwa upatikanaji wa mafuta yanayotosheleza mahitaji ya nchi na yenye viwango vya ubora unaotakiwa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) Bw. Erasto Simon, akizungumza leo Jijini Dar es salaam na Jukwaa la Wahariri Tanzania katika mkutano ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, amesema kuwa kwa sasa nchi inajitosheleza kwa nishati ya mafuta.
Bw. Simon amesema kuwa nchi inatumia zaidi ya lita milioni-15 za nishati ya mafuta na chini ya mfumo huo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja, umeleta unafuu wa gharama za uletaji wa mafuta na umesaidia kuokoa shilingi bilioni-500 kila mwaka kupitia mfumo wa BPS.
“Mfumo umesaidia kuongezeka kwa mapato ya kikodi yatokanayo na mafuta, kupunguza vitendo vya ukwepaji kodi kutokana na udanganyifu uliokuwa unafanywa, na kuthibiti udanganyifu katika gharama za mafuta katika soko la dunia” amesema Bw. Simon.
Amesema kuwa umesaidia kupunguza msongamano wa meli bandarini na kupungua upotevu wa mafuta wakati kwa kupakua mafuta kutoka meli.
Amefafanua kuwa wastani wa tani 1,100 huokolewa kila mwezi sawa na shilingi bilioni-4.16 kwa bei ya kikomo ya mwezi Disemba mwaka huu.
Bw. Simoni amesema kuwa lengo ni kuhakikisha mafuta wakati wote yanakuwepo ili kuendeleza uchumi katika nyanja mbalimbali.
Amesema kuwa serikali itaendelea kusimamia uingizaji wa mafuta ili yafanyike kwa uhalisia na kuleta tija kwa Taifa.
“Tukumbuke wadau wakubwa ni taasisi za serikali pamoja na makampuni ya mafuta zaidi ya 50” amesema Bw. Simoni.