Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi za elimu Tuamini, Modest Bayo akizungumza katika mahafali hayo mkoani Arusha.
Afisa Mtendaji mkuu wa benki ya uchumi kanda ya kaskazini,Samweli Wado akizungumza katika mahafali hayo.
Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Tumaini Senior iliyopo Makuyuni mkoani Arusha.
…………..
Julieth Laizer, Makuyuni.
Wahitimu wa kidato cha nne nchini wametakiwa kuendeleza ndoto zao kwa kujiendeleza zaidi kimasomo kwani elimu waliyoipata ni mwanzo tu kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yaliyopo hivi sasa.
Hayo yamesemwa na Afisa mtendaji mkuu wa benki ya uchumi kanda ya kaskazini, Samweli Wado wakati akizungumza katika mahafali ya tano ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Tumaini Senior iliyopo wilayani Monduli mkoani Arusha .
Aidha amewataka wahitimu hao kujipanga zaidi kwani elimu waliyoipata ni ndogo huku ikilinganishwa kuwa nchi sasa hivi inahitaji wasomi hasa waliobobea katika maswala mbalimbali ya sayansi na teknolojia huku na kupongeza shule hiyo kwa kufanyia kazi mtaala mpya wa elimu .
“napongeza shule hii kwa kufanya vizuri kitaaluma ikiwemo kufuata nyendo za serikali kielimu hususani katika mtaala mpya kwani Wahitimu wa kidato Cha nne wameonyesha mambo mazito ambayo ndio mpango halisi wa serikali kitaaluma kutokana na uelewa mkubwa na natoa wito kwa shule nyingine kuiga mfano huu.”amesema .
Pia aliwataka wanafunzi kufahamu umuhimu wa kujiwekea akiba katika maisha yao kwani ni faida kubwa na kufahamu nidhamu ya kutunza fedha, ambapo aliwapongeza Wahitimu Kwa kuonyesha Kwa vitendo yale waliojifunza zikiwemo tafiti mbalimbali za kuisaidia jamii ya kitanzania.
“Tumieni changamoto kama fursa na kubakia kihalisia zaidi na haikikisha Kila siku unaongeza kitu kipya ili kukua kuelekea katika mafanikio Yako.
Aliwaasa kumtanguliza Mungu mbele na kuendelea iumtegemea Mungu kama ambavyo maandiko matakatifu yanavyoelekeza.”amesema.
Aliwashukuru waalimu Kwa kuwapatia maarifa mazuri ambapo aliwaasa wazazi kwenda kuwaandikisha watoto kwa wingi Tumain Senior kwani shule hiyo inajali masilahi ya watoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi za elimu Tumaini Modest Bayo aliwataka Wahitimu kujipanga kuendelea na masomo yao ya kidato cha tano kwani bado hawajakamilisha ndoto zao kufuatia watoto hao kuhitajika kusoma mpaka elimu ya vyuo vikuu.
Aidha Wahitimu wa kidato Cha nne wamethibitisha namna ambavyo shule ya Tumain Senior inawanoa wanafunzi kitaaluma na kimaadili.
Kadhalika mkurugenzi huyo aliwaasa wazazi kuendelea kutoa ushirikiano Kwa waalimu ili kuwasaidia watoto wazidi kufanya vizuri katika masomo yao.
Alisema kuwa shule ipo katika mikono salama na pia kuhusiana na mtaala mpya utalenga zaidi kumsaidia mwanafunzi kujitegemea badala ya kuwa tegemezi ambapo mwanafunzi atanufaika na masomo kulingana na mazingira ikiwa mwanafunzi anatoka katika jamii ya kifugaji basi atafundishwa hivyo na ikiwa anatoka katika maeneo ya kilimo basi afanye kilimo cha kisasa zaidi.
Pia miradi mbalimbali ikiwemo masomo ya muziki yaliyopo kwenye somo la PBL ambalo amewataka wazazi kuendelea kuwaamini. na kuwaleta wanafunzi.
Tumaini inategemewa kuwa shule ya kwanza kuunga mkono mtaala mpya kwani tayari walishaanza mapema hivyo wazazi waendelee kuwaandikisha wanafunzi katika shule za Tumaini.
Hata hivyo katika kutatua changamoto ya uhaba wa maji shule wazazi Kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali ambao ni marafiki wameweza kupata zaidi milioni mbili huku mahitaji yakiwa ni milioni 3 lengo ni kuhakikisha huduma za maji zinakuwepo wakati wote.
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo ya Tumaini senior Sifael Msengi amesema kuwa katika Mahafali hayo ya 5 jumla ya Wahitimu 45 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu elimu ya kidato Cha nne.