Mkuu wa Idara ya Uanachama na Masoko kutoka Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi. Patricia Chao akimkabidhi Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bw.Adora Duwe kombe la MSD kuwa mshindi wa pili kundi la Mwajiri Bora wa mwaka 2023
MSD ilikuwa ni miongoni mwa taasisi za umma zilizoshiriki mashindano hayo ambapo pia taasisi binafsi zilihusishwa.
Mashindano hayo yanalenga waajiri kuboresha usimamizi wa rasilimali watu katika jukumu la kufikia malengo mkakati ya taasisi husika.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD Mboyi Wishega amesema tuzo hiyo ni chachu ya kuhakikisha tunaendelea kuzingatia misingi bora ya usimamizi wa rasilimaliwatu kwa ajili ya kuongeza tija kufikia malengo ya taasisi.