VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini katika kuendelea kuboresha sekta ya afya kwa wananchi wake leo amekabidhi rasmi gari maalumu aina ya Land cruser kwa ajili ya kusaidia shughuli mbali mbali katika Hospitali teile ya rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Koka amekabidhi gari hilo kwa niaba ya serikali ya awamu ya sita ikiwa zimetolewa na Rais DKt. Samoa Suluhu Hassan kwa lengo la kuweza kusaidia masuala mbali mbali ya afya katika hospitali hiyo ya Tumbi.
Alisema kuwa gari hiyo ambayo imetolewa na Rais itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kuongeza ufanisi zaidi katika suala zima la kuwahudumia wananchi pamoja na kutimiza wajibu wao
Pia alisema katika hospitali ya Tumbi bado inskabiliwa na changamoto ya usafiri kwa wagonjwa wanaokwenda kutibiwa hivyo amesema atalivalia njuga na kulipambania jambo hilo kwa kushirikiana na serikali.
Katika sherehe hiyo ya makabidhiano ambayo imehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali,madaktari pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) sambamba na wananchi.
Pia Koka alibainisha kwa kipindi cha miaka miwili na nusu wamepokea shilingi bilioni 6.8 ambazo zimeletwa katika kibaha mji kwa ajili ya kuboresha huduma ya afya na kuweza kufanya mambo mbali mbali ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba pamoja na kufanya ukarabati wa miundombinu ya majengo ya dharura na wagonjwa mahututi.
“Kwa kweli napenda kumshukuru kwa dhati Rais wa awamu ya sita DKt kwa kutoa fedha ambazo kwa kiasi kikubwa zimeweza kusaidia mambo ya kuboresha huduma katika hospitali ya Tumbi,”alisema Koka.
Kadhalika alisema Rais wa awamu ya sita ameweza kupambana kwa ajili ya kutoa fedha kwa lengo kufanikisha kujenga miradi mbali mbali ikiwemo zahanati na vituo vya afya.
Alisema kuwa ili kuweza kuleta mafanikio makubwa katika huduma ya afya ni lazima kufanya kazi kwa bidii kuanzia ngazi za chini lengo ikiwa ni kuwapatia wananchi huduma bora ya afya.
Mbunge huyo alisema lengo lake kubwa ni kuhakikisha anaboresha zaidi huduma ya afya na kwamba alishawahi kuchangia vifa tiba mbali mbali kwenye kituo cha afya mkoani vilivyogharimu milioni 700.
Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Amani Malima alisema kwamba gari hilo litaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuendeshea shughuli mbali mbali za kuwahudumia wagonjwa.
Aidha Mganga huyo alisema kuwa Hospitali hiyo ya tumbi ambayo ilianzishwa mnamo mwaka 1967 imekuwa ikiwaudumia zaidi ya wagonjwa 500 kwa siku hivyo kunahitajika magari zaidi ya kutolea huduma.
“Tunamshukuru sana Rais wetu kwa juhudi zake kwa kuweza kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa gari hii ambayo itasaidia kumaliza changamoto mbali mbali za usafiri kwa watumishi na wagonjwa.
Kadhalika alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha kwa kuweza kuwa mstari wa mbele kuwatumikia wananchi na kuwapambania kwa hali na mali katika kuwawekea mazingira mazuri ya kupata matibabu.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la elimu Kibaha Robert Shilingi alibainisha uwepo wa huduma wa gari hilo jipya ni moja ya hatua kubwa ya kuchochea kasi ya huduma ya usafiri kwa wagonjwa na watumishi.
Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani tumbi ilianzishwa mnano mwaka 1967 ambapo mwakw 2011 ilipandishwa hadhi ambapo kwa sasa inahudumia wagonjwa zaidi ya 500 kwa siku na kwa sasa ina jumla ya magari 6 ya kutolea huduma.