Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akizungumzana Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofuwa Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Onaeli Shoo kabla ya Ibada yaMaalum ya Kuaga Mwili wa Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto Kweka katikaUsharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro leo Desemba 5, 2023.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akitoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Baba Askofu Mstaafu, Dkt.Erasto Kweka, kabla ya Ibada Maalum ya Kuaga Mwili wa Baba Askofu leo Disemba 5, 2023 Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko Akiaga Mwili wa Marehemu Baba Askofu Mstaafu Dkt. Erasto Kweka, wakati wa Ibada Maalum ya Kuaga Mwili leo Disemba 5, 2023 Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.
……
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoawito kwa viongozi mbalimbali serikalini kuhakikisha kuwa, kaziw alizonazo wanazifanya kwa bidii kubwa na kuacha alama nzuri kwaw ananchi, hivyo ni muhimu kazi hizo zikaonekana na kufaidisha wananchi.
Amesema hayo tarehe 5 Desemba 2023 wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ibada Maalum ya kuaga Mwili wa Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto Kweka iliyofanyika katika Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.
Ibada hiyo Maalum ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Jerry Silaa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu.
“Nikitolea mfano wa Marehemu Baba Askofu Kweka ameacha alama nzuri duniani kwani ameanzisha vitu vingi ambapo hata kama ameondoka, vitu hivyo vinaendelea kuonekana na kufaidisha wengine mfano wa enzi ya uhai wa Baba Askofu alitoa mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya
kijamii ikiwemo kuleta usawa wa kijinsia, uanzishwaji wa miradi ya maji safi ndani na nje ya Dayosisi, Elimu, uanzishwaji wa Chama cha Akiba na Mikopo pamoja na Benki ya Uchumi ya KKKT ambayo inawahudumia watu wote na madhehebu yote.” Amesema Dkt. Biteko.
Dkt. Biteko ametoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kutokuta tamaa, akitolea mfano wa maisha ya Marehemu Baba Askofu
Kweka ambaye alianza kutafuta maisha akiwa kijana mdogo baada ya kufiwa na Baba yake akiwa na umri wa miaka 14 mpaka hatua aliyofikia sasa ya mafanikio kwa Kanisa la KKKT na watu wanapata huduma kupitia juhudi zake.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Samia Suluhu Hassan anatambua mchango wa Marehemu Baba Askofu Kweka kwenye maendeleo ya Kanisa la KKKT na kwamba Serikali itauenzi mchango wake katika Sekta pia za Afya, Elimu na Maji.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini , Dkt. Fredrick Onaeli Shooa amesema kuwa, viongozi wa Kanisa hilo wamefarijika na uwepo waviongozi wa Serikali waliojumuika nao kutoka siku msiba ulipotokea
mpaka wakati wa Misa hiyo Maalum.
Pia ametoa pole kwa Wananchi na Serikali kufutia maafa yaliyotokea
katika Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara ambapo baadhi ya wananchi
wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa kufuatia maporomoko ya ardhi
na ameeleza kuwa Kanisa linafarijika na juhudi mbalimbali
zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika
kutatua changamoto katika eneo hilo, na tayari Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa Majaliwa yupo katika eneo la maafa na timu kutoka kwenye
ofisi yake.
Marehemu Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto N. Kweka alizaliwa tarehe
24 Aprili, 1934 katika Kijiji cha Mamba Uswaa wilaya ya Hai mkoa wa
Kilimanjaro ambapo enzi ya uhai wake alitumika katika nyanja
mbalimbali ikiwemo Ualimu, kabla ya kuingia ngazi ya Utumishi wa
Kanisa.
Mwaka 1973 alichaguliwa kuwa Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya
Kaskazini wadhifa alioutumikia hadi mwaka 1976, ambapo mwaka mmoja
baadaye alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini na pia
kukaimu nafasi ya Mkuu wa Kanisa kabla ya kustaafu kwa heshima mwaka
2004
Marehemu Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Kweka alifariki Jumamosi tarehe 25
Novemba, 2025 saa 4 Asubuhi akiwa na umri wa miaka 89.
Captions
moja
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akizungumza
na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu
wa Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Onaeli Shoo kabla ya Ibada ya
Maalum ya Kuaga Mwili wa Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto Kweka katika
Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro leo Desemba 5, 2023.
Mbili
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akitoa
salamu za pole kwa familia ya Marehemu Baba Askofu Mstaafu, Dkt.
Erasto Kweka, kabla ya Ibada Maalum ya Kuaga Mwili wa Baba Askofu leo
Disemba 5, 2023 Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.
Tatu
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko Akiaga
Mwili wa Marehemu Baba Askofu Mstaafu Dkt. Erasto Kweka, wakati wa
Ibada Maalum ya Kuaga Mwili leo Disemba 5, 2023 Usharika wa Moshi
Mjini mkoani Kilimanjaro.