Waziri wa Fedha na Mipango Tanzania Mwigulu Nchemba ,Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt.Saada Mkuya wakibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Nathan Belete wakati wakimpokea Rais wa Benki ya Dunia kuelekea Mkutano Mkuu wa IDA 20 unaotarajiwa Kufanyika kesho Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Rais wa Benki ya Dunia Ajaya Banga akisalimiana na Viongozi mbalimbali waliofika kumpokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati alipowasili kuelekea Mkutano wa Tathmini ya Utekelezaji wa Mzunguko wa 20 wa Mfuko wa IDA unaotarajiwa kufanyika kesho Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Rais wa Benki ya Dunia Ajaya Banga akipokelewa kwa ngoma ya Msewe wakati alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kuelekea Mkutano wa Tathmini ya Utekelezaji wa Mzunguko wa 20 wa Mfuko wa IDA unaotarajiwa kufanyika kesho Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Rais wa Benki ya Dunia Ajaya Banga akiwa na ujumbe wake wakibadilishana mawazo na Watendaji wa Wizara ya Fedha mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kuelekea Mkutano wa Tathmini ya Utekelezaji wa Mzunguko wa 20 wa Mfuko wa IDA unaotarajiwa kufanyika kesho Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Juma Malik Akil akitoa taarifa kwa vyombo vyab habari kuhusiana Mkutano wa Tathmini ya Utekelezaji wa Mzunguko wa 20 wa Mfuko wa IDA unaotarajiwa kufanyika kesho Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
……..
Na Fauzia Mussa, Maelezo
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua Mkutano wa mapitio wa muhula wa kati wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa AIDA20 unaotarajiwa kufanyika kesho Disemba 06 Visiwani Zanzibar.
Akitoa taarifa Kwa vyombo vya habari kuhusiana na Mkutano huo huko Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Juma Malik Akili amesema, Mkutano huo utajadili Utekelezaji wa miradi ya IDA20 na kutafakari juu ya miradi ya IDA21 Kwaajili ya maendeleo ya kimataifa.
Alisema Kufanyika kwa Mkutano huo ndani ya Zanzibar kutasaidia kuitangaza Zanzibar katika utalii wa mikutano na kupelekea ongezeko la watalii wanaoingia Nchini.
Amesema Zanzibar inatekeleza miradi mbali mbali ya Benki ya Dunia ikiwemo miradi ya Miundombinu na miradi ya uchumi wa buluu ambayo kupitia mkutano huo itafanyiwa tathmini na kuangaliwa wapi imefikia pamoja na changamoto zinazoikabili na kuzipatia ufumbuzi.
Amefahamisha kuwa, pamoja na Mkutano huo Rais wa Benki ya Dunia Ajaya Banga na ujumbe wake watapata fursa ya kutembelea maeneo mbali mbali yanayotekeleza miradi ya IDA ikiwemo Bumbwini, ,Muungoni na Jang’ombe kwa lengo la kukutana na wanufaika wa miradi hiyo pamoja na kuangalia athari za mabadiliko ya msaada wa IDA.
Mkutano huo wa siku 3 unafanyika kwa mara ya kwanza visiwani Zanzibar na kushirikisha a na wajumbe kutoka Nchi mbali mbali Duniani.