Na Issa Mwadangala
Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo Disemba 04, 2023 baada ya kupata elimu na kujengewa uelewa kuhusu umuhimu wa kuwa karibu na Polisi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za ukatili na vitendo vingine vya kihalifu elimu ambayo ilitolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya ikiwa ni muendelezo wa dhana ya ushirikishwaji wa jamii kwa makundi yote kwa lengo la kufichua na kudhibiti uhalifu mkoani Songwe.
Aidha, Kamanda Mallya aliwasihi wanafunzi hao kuacha kupokea zawadi kwa watu wasiowafahamu pia kukataa kutumwa na watu wasiowafahamu ikiwemo kuacha kudhulura hovyo na kutembea usiku wakiwa peke yao ili kuepuka kufanyiwa vitendo vya ukatili