Awamu ya ya kwanza vya vifaa tiba na dawa vilovyotolewa na serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko Hanang imewasili katika Hospitali ya Wilaya ya Hanang (Tumaini).
Meneja wa Kanda ya MSD Kilimanjaro Rehema Shelukindo ameeleza kuwa, vifaa hivyo ni pamoja na maji ya drips, dawa za kuponya magonjwa ambukizi na mengineyo(antibiotics), dawa za msumivu na mashuka.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai ameeleza kuwa MSD itaendelea kupeleka bidhaa za afya katika eneo hilo kadri inavyoelekezwa na serikali.