Adeladius Makwega –MWANZA
Wakristo wameambiwa kuwa njia pekee ya kuwaweka huru na njia ya itakayowaweka katika mazingira mazuri ni kutembea katika maagizo ya Mungu,“Ndiyo maana katika injili ya leo ya Marko 13:33-37 tunaambiwa kuwa tunatakiwa kukesha maana yeye anakuja kwetu, kwa wale atakaowakuta wakikesha atawapa tuzo, siku hiyo atakayakuja hatuidhanii ili aje kutoa hukumu ya haki.”
Hayo yamesemwa na Padri Samson Masanja, Paroko wa Parokia ya Malya Katika Kanisa la Bikira Maria Malkia wa Wamisionari-Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, katika misa ya kwanza ya dominika ya kwanza ya majilio ya mwaka B wa Liturjia ya kanisa, Disemba 3, 2023.
Misa hiyo pia ilikuwa na nia na maombi kadhaa,“Utusaidie kutambua kuwa maisha yetu ni kama mkopo ambao tunaotakiwa kuurejesha, Eee Bwana Twakuomba utusikie.”
Hadi misa hiyo inamalizika majira ya saa moja ya asubuhi, hali ya hewa ya Malya na viunga vyake ilikuwa ya mvua ambao mara baada ya misa hii kumalizika mvua ilinyesha, huku waamini walitoka kanisa kuelekea majumbani wakisindikizwa na mvua hiyo.
Wakati mvua hiyo inanyesha baadhi ya wakulima waliopanda mahindi Septemba, 2023 sasa wanayakwanyua na kuchemsha au kuyachoma huku wakulima wengine wakipanda mahindi pia.