Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Massoud Othman akihutubia katika maadhimisho ya Kitaifa ya siku ya watu wenye ulemavu yanayofanyika Disemba 3 Duniani kote,huko Ukumbi wa Polisi Ziwani.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akimkaribisha Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Massoud Othman kuhutubia katika maadhimisho ya Kitaifa ya siku ya watu wenye Ulemavu yanayofanyika Disemba 3 Duniani kote,huko Ukumbi wa Polisi Ziwani.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika maadhimisho ya Kitaifa ya siku ya watu wenye ulemavu yanayofanyika Disemba 3 Duniani kote,huko Ukumbi wa Polisi Ziwani.
Mkalimani wa lugha za alama kutoka JUWALAZA Mohammed akiwasaidia uelewa watu wenye ulemavu wa uziwi katika maadhimisho ya Kitaifa ya siku ya watu wenye ulemavu yanayofanyika Disemba 3 Duniani kote,huko Ukumbi wa Polisi Ziwani.
Mwenyekiti wa Baraza la Watu wenye Ulemavu Zanzibar Salma Haji Saadat akizungumza katika maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu yaliyofanyika Ukumbi wa Polisi Ziwani.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Magharibi Simai Msaraka akitoa salamu kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa maadhimsho ya Kitaifa ya siku ya watu wenye ulemavu yaliyofanyika Ukumbi wa Polisi Ziwani.
.……………………….
Na Rahma Khamisi Maelezo 3 /12/2023
Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe, Othman Masoud Othman ameitaka jamii kuwaenzi ,kuwalinda, na kuwatetea watu wenye Ulemavu ili kuwaepusha na vitendo vya udhalilishaji.
Wito huo ameutoa katika Ukumbi wa Polisi Ziwani wakati akizungumza na wananchi katika maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani.
Amesema kuwalinda na kuwatetea Watu hao si jambo la hiari bali ni maamuzi ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ambayo inaitaka Serikali na jamii kwa ujumla kuwasadia watu hao.
“ kuwasadia watu wenye ulemavu ni jambo la lazima kwa jamii na Serikali kwani wanahitaji huduma zote muhimu bila ya ubaguzi ikiwemo afya na miundombinu wezeshi.”alisema Mhe,Othman
Aidha amefahamisha kuwa Serikali itahakikisha kuwa hakuna anaechwa nyuma katika maendeleo na itaendelea kushirikiana na watu hao ili kuwawezesha kufikia malengo yao.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetenga bajeti katika mfuko wa Maendeleo ya Watu Wenye Ulemavu kwa dhamira ya kutoa msukumo na kuimarisha ustawi kwa kujumuisha huduma za Afya,Elimu ,Marekebisho na Ununuzi wa Vifaa saidizi .
“Serikali inachukua juhudi mbalimbali kwa watu wenye ulemavu ili kutataua changamoto zinazowakabili hasa katika mikopo ya uzalishaji wasione wameonewa kwani sisi tunaendelea kujitahidi ili kuzitafutia ufumbuzi “alifahamisha Makamo wa Kwanza wa Rais.
Hata hivyo amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawaandikisha watoto wenye ulemavu maskulini ili kuhakikisha wanapata haki yao ya elimu.
Nae Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wenye Ulemavu Salma Haji Saadat amesema watu wenye ulemavu wanahitaji kuwezeshwa kwa kupatiwa mikopo ili wajiendeleze kiuchumi kwani na wao wana haki kama watu wengine.
Aidha amesema kuwa ujumbe wa mwaka huu umeenda sambamba kwani unahimiza haki za watu wenye Ulemavu hivyo ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha kwamba wanawathamini na kuwajali watu hao.
Akisoma risala Makamo Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Wenye Ulemavu Ali Omar ameiomba Wizara husika kuwajengea Skuli za wanafunzi wenye Ulemavu yenye vifaa vya kutosha ili kusoma kwa ufanisi zaidi.
Aidha ameiomba Serikali kuzingatia usalama wa watu wenye ulemavu kwa kuwekewa miundombinu rafiki ya barabara ili waweze kutembea bila ya wasiwasi.
Aidha amefahamisha kuwa Watu wenye ulemavu ndio maskini wakubwa wa kufikia malengo hivyo wameiomba Serikali kuwajengea miundombinu mahususi ya kiuchumi ili waweze kufanya biashara ili kujikwamua na umaskini.
Maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu huadhimishwa kila ifikapo Desemba 3 ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu ni “tuungane kuchukua hatua katika kutoa Huduma ili kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa Watu Wenye Ulemavu”