Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda amesema historia ya Bibi Titi wanawake na wananchi wanajifunza mengi kuhusu uzalendo kwa nchi yao, uwezo na nafasi ya mwanamke kwenye jamii, mchango wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi kwenye Taifa hili.
Akizungumza leo Katika Kongamano la Bibi Titi Mohamed Mwenyekiti Chatanda amesema sisi Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) hivi karibuni tunatarajia kuandaa Tamasha la kuwatambua Wanawake wote waliothubutu kusimama na kushirikiana na viongozi wengine wa Taifa hili kutoa Mchango wenye mafanikio makubwa kwa Taifa letu.
Mwenyekiti Chatanda amesema kuanzishwa kwa UWT ni kumkomboa mwanamke dhidi ya ubaguzi wa kifursa, ukatili wa kijinsia na udumavu wa kifikra,Leo tunasherekea Tamasha hili mahususi la kumuenzi Binti Titi kwa kupitia midahalo hiyo kizazi cha sasa kitamfahamu vizuri Wasifu wa Bibi Titi,na hapa niwasihi vijana muwe na utamaduni wa kusoma vitabu mbalimbali vya kihistoria kikiwemo kitabu cha Wanawake wa Tanu , Jinsia na Utamaduni katika kujenga Uzalendo Tanganyika 1955 -1965 utathibistisha kuwa Bibi Titi alikuwa na kipawa cha kipekee ya ushawishi katika harakati za kutafuta Uhuru.
Mwenyekiti Chatanda amesema niwapongeza sana kwa kuandaa Tamasha hili ili vijana wa sasa ,wanaRufiji na Watanzania kutumia vizuri vipawa tulivyojaaliwa ikiwemo wenzetu wasanii kuijenga nchi yetu, kuonesha mazuri yanayofanywa ndani ya nchi yetu, kukuza tamaduni zetu nzuri za kitanzania kuwaunga mkono na kuwatia moyo viongozi wa Nchi yetu akiwemo Mbunge wa Jimbo hili la Rufiji aliaminiwa na kuteuliwa kuwa Waziri na siku zote amekuwa akifanya kazi nzuri, hongera sana.
“Bibi Titi Mohamed tunayemuenzi leo hapa Rufiji, ndiye aliyekuwa Mwanamke wa kwanza na Mbunge wa Kwanza wa Jimbo la Rufiji mara baada ya Uhuru,hivyo tunampongeza Mheshimiwa Mchengelwa kwa kuendelea kumuenzi Bibi Titi kwa vitendo kupitia kazi mbalimbali unazozifanya ndani ya Jimbo la Rufiji na Taifa kwa ujumla ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Chetu Cha Mapinduzi, na nyinyi wananchi ni mashahidi mnashuhudia miradi mingi ya Maendeleo inatekelezwa Jimboni ikiwemo ujenzi wa mradi wa kufua umeme, unaogharimu takribani Trioni Sita ,miradi ya sekta ya miundombinu ya barabara,sekta ya Elimu, Afya”.