NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani katika kuanza wiki ya shukrani kwa mlipa kodi imeamua kurudisha fadhila kwa jamii kwa kutoa msaada wa vifaa mbali mbali vya ujenzi kwa ajili ya kuendeleza mradi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika zahanati ya Misugusugu halmashauri ya mji Kibaha.
Akizungumza katika halfa ya kukabidhi msaaada wa vifaa hivyo Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani Masawa Masatu alisema kwamba wameamua kusapoti sekta ya afya kwa lengo la kuweza kuwakomboa wakinamama kupata huduma bora hasa wakati wa kujifungua.
Meneja huyo alibainisha kwamba TRA katika zahanati ya misugusugu kuna changamoto ya miundombinu ya jengo la mama na mtoto hivyo wakaona kuna umuhimu wakusaidia vifaa hivyo ambavyo vitasaidia katika ujenzi huo.
“Tupo katika wiki ya shukrani kwa mlipa kodi na sisi kama TRA Mkoa wa Pwani tumeona ni vuzuri tukaungana na wananchi katika ujenzi huu ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa changamoto ya wakinama kupoteza maisha yao hasa wakati wa kujifungua,”alisema Masatu.
Meneja alisema kuwa ana imani msaada huo utaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa wanawake wa kata ya misugusugu na maeneo mengine kuweza kupata fursa ya kuweza kuondokana na usumbufu waliokuwa wanaupata katika kipindi cha nyuma.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii wa kata hiyo, Kezia Olambo aliwashukuru kwa dhati TRA kwa msaada huo wa kuisaidia jamii katika suala zima la kuboresha sekta ya afya.
Alisema wananchi wa kata hiyo wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za mama kujifungua katika eneo la Mlandizi na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Pwani ya Tumbi jambo ambalo limekuwa likichangia kuongea Vifo vya mama na mtoto.
“TRA tunawashukuru Kwa kutupatia msaada wa vifaa hivi vya ujenzi maana ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika zahanati hii itaokoa maisha ya wanawake wanahitaji huduma ya kujifungua maana wengi wamekuwa wakitoka hapa kwenda kufuata huduma mlandizi au hosptali ya rufaa ya mkoa wa Pwani”alisema
Naye Afisa mtendi wa kata hiyo, Elizabeth Mwakalikwa, alisema ujenzi wa jengo Hilo utagaharimu zaidi ya shilingi milioni 60, na kwamba bado jitihada za makusudi zinahitajika ili kumalizia ujenzi huo na kuwaomba wadau wengine kujitokeza ili kukamilisha mradi huo.
“TRA wametupatia msaada na tunamshukuru na kupitia msaada huu tutaendelea kuhamasisha wananchi kulipa Kodi Kwa ajili ya maendeleo yetu wenye…ujenzi huu bado haijakamilika tunaomba wadau wengine wajitokeze kutoa misaada ambayo itusaidia”alisema
Swaiba Kaisi mkazi wa kata ya misugusu, alisema kukamilika Kwa ujenzi wa jengo Hilo litakuwa mkombo Kwa wanawake kuondokana na adhamba ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma umbali mrefu ambapo utapunguza vifo vya wanawake wajawazito.
Katika hatua nyingine mamlaka hiyo imetoa msaada wa vyakuka na vinywaji katika kituo Cha watoto yatima cha Fadhillah Ophanage Center ambayo ni, sabuni, unga, Mchele, mafuta, sukari na mahitaji mengi ya msingi.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ya mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa Pwani katika wiki ya shukrani kwa mlipa kodi inasema kodi yetu maendeleo yetu tuwajibike.