Na Sophia Kingimali,Dar es salaam
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amelitaka Shirika la Umeme TANESCO kuhakikisha wakandarasi wanaopewa mikataba ya kusambaza vifaa vya kufanya matengenezo kwenye njia za umeme wafanye kazi kulingana na mikataba yao na wazembe kutokuendelea nao pindi mikataba yao itakapoisha
Hayo ameyasema leo Desemba 1,2023, jijini Dar es salaam alipotembelea kituo cha kupoozea umeme ilala lengo likiwa kuangalia uendelezaji wa mradi wa kuweka njia ya umeme ardhini kutokea ilala kwenda kurasini.
Amesema TANESCO wanapaswa kuhakikisha vifaa vya kurekebishia njia za umeme zinazopeleka kwa wananchi ambazo zinasumbua vinapatikana kwa wakati na kumaliza tatizo hilo.
“Niwaelekeze TANESCO hakikisheni mnatillia mkazo mikataba hiyo ili vifaa vipatikane kwa wakati vifaa vimekua vinasumbua lakini vilevile hawa wasambazaji wengine ambao wapo kwa muda mrefu wanasumbua na hawachukuliwi hatua tutaanza pamoja na wao”amesema Kapinga.
Amesem kutokana na ukubwa wa mji pamoja na mahitaji yake endapo wahusika hawatachukuliwa hatua kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao itaendelea kuleta athari kwa wananchi.
Amesema serikali inatoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi sasa wataanza kuchukua hatua kwa wakandarasi wote ambao wameshindwa kuendana na mikataba yao kwa sababu hakuna mtanzania anaeweza kukaa bila umeme.
“Serikali imetoa fedha nyingi sana kwa hiyo hatutaweza kuvumili njia za umeme zisiboreshwe kwa sababu ya uzembe wa watu wachache tunapaswa kufanya kazi hizi kwa weredi ili watanzania waweze kuchagiza shughuli zao za kiuchumi”amesema
Akizungumzia uendelezaji wa njia ya ardhini ya umeme amesema mradi huo utakapo kamilika utaondoa shida ya kukatika kwa umeme kwenye maeneo ya kigamboni,ilala,kurasini,Mbagala na Temeke ambapo limetokana na ongezeko la watu na makazi kwenye maeneo hayo.
Amesema kwenye maeneo hayo wananchi wamekua na changamoto ya kukatika kwa umeme pamoja na kuwa tatizo la umeme lililopo.
Amesema wanaendelea na maboresho ya vituo vyao ikiwemo kituo cha kupozea umeme cha Mbagala ili kuhakikisha tatizo la umeme katika maeneo hayo linaisha kabisa.
“Hata tukiwa na umeme wa kutosha lakini hatujaboresha njia za wananchi za kupata umeme wa uhakikia basi bado tutakua na changamboto kubwa”amesema
Aidha ameongeza kuwa serikali inafanya kila jitihada ili kuhakisha inaboredha hali ya upatikanaji wa umeme.
Kwa upande wake Mhandisi wa mradi Nicholas Anthony amesema mpaka sasa mradi umefikia asilimia 68.14 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi,2024.
Amesema mradi huo utakapokamilika utasaidia kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wilaya ya Temeke kwani maeneo hayo yatakuwa na umewezo wa kupokea umeme kutoka ubungo,kinyerezi,kipawa kwenda kurasini.
Mradi wa kusambaza njia za umeme ardhini kutoka ilala kwenda kurasini umefadhiriwa na serikali kwa asilimia 100 na mkandarasi anendelea na kazi ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi March,2024.