…………….
Kamishna wa Polisi Kamisheni ya Intelijensia ya Jinai CP Charles Mkumbo amewataka madereva wa vyombo vya usafiri kufuata sheria na kanuni za Usalama barabarani ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kusababisha kupoteza maisha na kupata ulemavu wa kudumu kwa watu na hivyo kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Aidha, amesema Jeshi la Polisi kama msimamizi wa sheria za usalama barabarani litasimama imara na kuhakikisha sheria zote za barabarani zinafuatwa pamoja na kuwachukulia hatua za kinidhamu madereva wakaidi.
Kamishna Mkumbo amesema hayo Disemba 1, 2023 Nzuguni, Jijini Dodoma alipokuwa akiaga mwili wa marehemu Godfrey Marco Chilya kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, marehemu ni mtoto wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma