Mwenyekiti wa Bodi Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) Bw. Dadala Chacha, Meneja Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Amani Nkurlu, Afisa Biashara Benki ya TADB Bw. Kezilahabi Jumanne, Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa ziara ya kuangalia miradi ya CHAURU ambao ni wanufaika wa Benki ya TADB iliyofanyika Novemba 30 /11/ 2023 katika Kijiji Cha Visezi, Kata ya Vigwaza, Chalinze Mkoa wa Pwani.
Meneja Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Amani Nkurlu akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika ofisi za Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) zilizopo katika Kijiji Cha Visezi, Kata ya Vigwaza, Chalinze Mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) Bw. Dadala Chacha akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu historia ya ushirika huo ulioanzishwa mwaka 2002 pamoja na changamoto wanazozipata ndani na nje ya ushirika huo.
Afisa Biashara Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Kezilahabi Jumanne akitoa ufafanuzi kwa Wahariri wa vyombo vya habari namna walivyowawezesha CHAURU kwa kuwapatia mkopo kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo cha umwagiliaji wa zao la mpunga.
Wahariri wa vyombo vya habari wakipewa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kutoka kwa uongozi wa Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) kuhusu utekelezaji wa majukumu yao.
Muonekano wa mashine ya kisasa ya kukoboa mpunga inayomilikiwa na Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) baada ya kupata mkopo kutoka benki ya TADB.
Mwenyekiti wa Bodi Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) Bw. Dadala Chacha (kulia) akiwaonesha wahariri wa vyombo vya habari pomoja na uongozi wa Benki ya TADB Shamba la Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji zao la mpunga katika Kijiji Cha Visezi, Kata ya Vigwaza, Chalinze Mkoa wa Pwani.
Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) pamoja na Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU)
…………
NA NOEL RUKANUGA, PWANI
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanikiwa kuwawezesha
Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) kwa kuwapatia mkopo wa shillingi bilioni 1.7 jambo ambalo limewasaidia kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga kutoka gunia 15 hadi 30 kwa ekari moja.
Uwezeshaji wa Benki ya TADB imeifanya CHAURU kufanya maboresho ya miundombinu ya shughuli za kilimo cha umwagiliaji, kununua mashine ya kisasa kukoboa mpunga pamoja na kupiga hatua kubwa ya uzalishaji na kufikia tani 5,000 kwa kila msimu.
Akizungumza na wahariri wa yombo vya habari Novemba 30, 2023 katika Kijiji Cha Visezi, Kata ya Vigwaza, Chalinze, Mkoa wa Pwani, wakiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya wanufaika wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Afisa Biashara Benki ya TADB Bw. Kezilahabi Jumanne, amesema kuwa ni jukumu lao kuchagiza shughuli za kilimo kwa kutoa mkopo kwa CHAURU ili kuongeza tija katika uzalishaji zao la mpunga.
Bw. Jumanne amesema kuwa benki TADB wakati inaaza kuwasaidia CHAURU mwaka 2008 walikuwa wanalima hekta 420 baada ya kuwapatia mkopo eneo la uzalishaji limeongezeka hadi kufikia hekta 720.
“Wamepiga hatua kubwa kwani wameweza kutoa ajira za kudumu kwa watu tisa ikiwemo kuajiri maafisa ugani ambao wamekuwa wakiwasaidia kutoa ushauri wa njia ya bora uzalishaji zao la mpunga kupitia kilimo cha umwagiliaji” amesema Bw. Jumanne.
Amesema kuwa la benki ya benki ya TADB kuona chama cha CHAURU kinaendelea kukua na kuleta tija kwa wakulima Mkoa wa Pwani.
“Tupo katika mpango wa kuwawezesha kupata gala kwa ajili ya kuifadhi mazao yao, kwa sasa wanauwezo wa kuifadhia tani 5,000 kutokana uzalishaji unaongezeka watamani kupata gala lenye uwezo wa kuzalisha tani 10,000” amesema Bw. Jumanne.
Mwenyekiti wa Bodi Chama Cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji (CHAURU) Bw. Dadala Chacha, amesema kuwa mkopo walioupata kutoka benki TADB umewasaidia kwa asilimia kubwa katika utekelezaji wa shughuli zao.
Bw. Chacha amesema kuwa mpaka sasa tayari wamefanya marejesho ya shilingi bilioni 1. 4.
“Mkopo wa Benki ya TADB umewasaidia wanachama wa CHAURU kwa kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga” amesema Bw. Chacha.
Bw. Chacha amesema kuwa wamefanikiwa kuboresha miundombinu ya mbalimbali ikiwemo umwagiliaji kwa kutumia shillingi milioni 500 pamoja na kununua pampu ya maji yenye thamani ya shilingi milioni 68.
“Sisi wanachama cha CHAURU tunawashukuru Benki ya TADB, hatuna cha kuwalipa ila tunaendelea kuwaombea watumishi wa benki kwa Mwenyezi Mungu ili waendelee kuwasaidia wakulima wengine kama walivyotusaidia sisi” amesema Bw. Chacha.
Bw. Chacha amesema kuwa CHAURU inajumla ya wanachama 900 ambapo kila mwanachama analima ekari mbili zao la mpunga.
Ametoa wito kwa wakulima nchini Tanzania kuchangamkia fursa katika Benki ya TADB kukopa fedha kwa ajili ya shughuli za kilimo cha kisasa pamoja na kufanya marejesho jambo ambalo linaleta tija ya kuwa na nidhamu ya fedha.
Nae Mkulima wa CHAURU Bi. Salim Sareh amesema kuwa kwa sasa wanaishi katika mazingira rafiki ya kibiashara tofauti na awali kutokana wanaweza kutatua changamoto za kifamilia ikiwemo kusoma watoto wao.
“Tumekuwa tukipewa mikopo ambayo inatusaidia katika shughuli za kilimo kwa sasa tunashuruku Mungu tunapata faida ambayo itasaidia kuendesha maisha yetu” amesema Bi. Sareh.
CHAURU ni Chama Cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu ambacho kinapatikana katika Kijiji Cha Visezi, Kata ya Vigwaza, Chalinze, Mkoa wa Pwani.
Chama hiki kilianzishwa mwaka 2002 na kusajiliwa kwa mujibu wa sheria namba 5 ya vyama vya ushirika na kupewa usajili namba CR 360 na shughuli yake kubwa uzalishaji wa mpunga kwa njia ya umwagiliaji.
CHAURU imekuwa ikichakata mpunga wa wakulima chenye uwezo kukoboa madaraja yote ambao unatokana na uzalishaji usiopungua tani 5,000 kwa msimu.