VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Selina Koka ametoa doti za vitenge 80 kwa ajili ya wanawake wa UWT Kibaha mji mkoani Pwani kwa lengo kushona sare kwa ajili ya kumuenzi Bibi Titi Mohamed.
Selina Koka ambaye pia mlezi wa umoja UWT Kibaha mjini amesema kwamba lengo lake kubwa ni kushitiki kikamilifu katika killed cha kumuenzi Bibi Titi kwa yale mambo mbali mbali mazuri ambayo ameyafanya katika Taifa la Tanzania.
Aidha Mama Koka alisema ameamua kutoa sapoti ya vitenge hivyo kwa wanawake wa UWT ili waweze kuungana kwa pamoja na wanawake wengine wa Mkoa wa Pwani na maeneo mengine katika sare ya pamoja ili waweze kukutana na kukumbuka yale mazuri ambayo ameyafanya katika nyanza mbali mbali.
“Tunatambua mchango mkubwa ambao ameufanya Bibi Titi Mohamed kwani alikuwa ni mwanamke wa kwanza kujiunga na harakati mbali mbali katika suala zima la kupigania uhuru wa Tanganyika kwa hivyo na sisi ni vema na sisi kama wanawake tumuenzi,”alisema Selina.
Kadhalika Selina aliwahimiza wanawake wengine wa UWT Kibaha mji kujitokeza kwa wingi katika kushiriki kikamilifu katika sherehe za kumuenzi Bibi Titi katika kilele ambacho kitafanyika Wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Kibaha mji Elina Mgonja amempongeza kwa dhati mke wa Mbunge kwa kujitoa kwake kwa hali na mali katika kuwasapoti kwa vitenge hivyo ambavyo vitawasaidia wawe katika sare ya pamoja.
Bibi Titi Mohamed ambaye alizaliwa mnamo mwaka 1926 katika jiji la Dar es Salaam na kufariki dunia Novemba 5 mwaka 2000 ambapo alishawahi kushika nafasi mbali mbali za chama pamoja na masuala mbali mbali ya harakati hasa kwa upande wa wanawake.