Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe ACP Theopista Mallya amewalisha keki wanafunzi wa shule ya msingi God’s bridge wakati wa mahafali ya kidato cha nne ya shule hiyo ya bweni ikiwa ni ishara ya upendo na urafiki kati ya wanafunzi hao na Jeshi la Polisi.
Kamanda Mallya, baada ya kupewa keki hiyo aliamua kuifungua na kuwagawia watoto wadogo wa shule ya Msingi ya God’s Bridge ambao pia waliohudhuria katika Mahafali hayo ili kuendelea kujenga na kuimarisha uhusiano na urafiki alitumia fursa hiyo kuwaonesha upendo kwa kula pamoja.
Aidha, kamanda Mallya mbali na kuwalisha keki pia aliwasisitiza kutosita kutoa taarifa mbalimbali za uhalifu ikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto.