Afisa elimu sekondari ,Abel Ntupwa akizungumzia matokeo ya darasa la saba ofisini kwake mkoani Arusha.
……..
Julieth Laizer, Arusha .
Arusha.Afisa Elimu Mkoa wa Arusha Abel Ntupwa amesema kuwa mkoa wa Arusha umepokea matokeo ya wanafunzi takribani 54,357 waliokuwa wamesajiliwa ambapo wanafunzi waliofanya mitihani ni wanafunzi wapatao 53,341 sawa na asilimia 98%.
Kutokana na sababu mbalimbali wapo wanafunzi wengine ambao hawakuweza kufanya mtihani ambao ni sawa na asilimia 2% na kusema hapa Kuna maboresho makubwa sana kwani huko nyuma wanafunzi mpaka asilimia 12%walikuwa hawafanyi mtihani.
Amesemakuwa kati ya wanafunzi 53341 wanafunzi waliofaulu na wenye sifa ya kuingia kidato Cha kwanza ni 45685.
Ufaulu huo ni sawa na asilimia 85.64 ambapo kama mkoa wamepiga hatua moja kwenda mbele kwani ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 1.66 ukilinganisha na matokeo ya mwaka Jana ya asilimia 83.3.
Ntupwa alisema kuwa halmashauri zimendelea kufanya vizuri sana kwani halmashauri ya jiji la Arusha imefaulisha Kwa asilimia 98.99 ambao ni ufaulu mkubwa sana ambapo ingedhaniwa Kuna halmashauri imeporomoka lakini bado ufaulu wake ni mkubwa kwani imefaulisha Kwa asilia 74%.
Alisema wanafunzi wapatao 45,685 serikali inaenda kuwapanga wote hao Kwa utaratibu maalumu kwenye mfumo na wale ambao watakaofaulu vizuri zaidi watapangwa na kupelekea shule za Bweni na hakuna ajuaye nani atakuwa wapi na yupi atakwenda wapi mgumu utawatambua na kuwabaini kulingana na uwezo walionesha.
Alisema kuwa watu wasidhani wataweza kuongea na maafisa elimu ama walimu kuwapanga watoto wao wasomee eneo fulani, alisema hii hali ya kupanga wanafunzi inafanyika kulingana mfumo.
Alitoa rai kwa wazazi kujipanga na maandalizi ya Watoto wao katika mahitaji ya kishule ifikapo mwakani januari 2024 .
Kwa upande wake serikali imejiandaa Kwa waalimu na miundo mbinu na Kwa karibu Kila hitaji kwani hata Sasa uandikishaji wa darasa la kwanza unaendeleaje hivyo wazazi na walezi wawapele watoto shule.