OR-TAMISEMI
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Dkt. Batilda Burian amewataka Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kuzuia migogoro kati ya Serikali na wananchi hasa migororo ya ardhi kwa kuwa mingi inaanzia kwenye ngazi zao.
Mhe. Burian ameyasema hayo leo alipokuwa akifunga Mafunzo ya viongozi hao yaliyofanyika kwa siku mbili mkoani humo.
Amesema migogoro ya ardhi imekuwa ni changamoto kubwa katika maeneo mengi na kuwaelekeza maafisa hao kua wazalendo na imani na kutumia misingi ya haki na sio upendeleo pale linapokuja suala la uuzaji wa ardhi za watu.
“Baadhi ya vijiji wameuza ardhi na wananchi wanalalamika hii inasababisha baadae migogoro kati ya Serikali na wananchi wake mnapaswa kuwa na maadili mnapotekeleza majukumu yenu,”amesema.
Aidha, amesisitiza viongozi hao kuwa na ushirikiano mzuri na wananchi wanaowaongoza kwenye maeneo yao.