Na Mwandishi Wetu.
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba nchini (TMDA), kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wake, Bw. Adam Fimbo leo Novemba 27,2023 imetolea ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya uwepo wa dawa aina ya Carbotoux (Carbocisteine 100mg + Promethazine 2.5mg)
Dawa hiyo, inayotengenezwa na Kampuni ya Labotatories P.P.M, Cambodia katika soko la Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo imebainisha kuwa:
“Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikihusisha kuwepo kwa dawa duni yenye jina Carbotoux (Carbocisteine 100mg + Promethazine 2.5mg)katika soko la Tanzania.
“Taarifa hiyo, inaainisha kuwa dawa tajwa husababisha madhara makubwa kwa watumiaji na hivyo sio salama kwa matumizi ya binadamu.
Hata hivyo, TMDA inapenda kutoa ufafanuzi na kuuhakikishia umma kuwa dawa yenye jina Carbotoux haijawahi kusajiliwa kwa matumizi hapa nchini.
Vilevile, kampuni ya Labotatories P.P.M, Cambodia inayotengeneza dawa hiyo, haijasajili dawa yoyote hapa nchini.”Imebaimisha taarifa hiyo ya Mkurugenzi Mkuu wa TMDA , Adam Fimbo.
Aidha,Pamoja na ufafanuzi huo, TMDA imesajili dawa zenye kiambata cha Carbocisteine + Promethazine, zinazotengenezwa na makampuni mengine. Dawa hizo ni bora, salama na fanisi kwa matumizi yaliyokusudiwa.
“Mamlaka imeimarisha udhibiti wa mifumo ya ufuatiliaji wa dawa katika soko (post marketing surveillance) ili kuweza kubaini uwepo wa dawa duni zikiwemo ambazo hazijasajiliwa na Mamlaka.”Amebainisba Sha kwenye taarifa hiyo .
Hata hivyo, TMDA imewataka Wananchi kutoa ama kuwezesha taarifa kupitia namba ya bure 0800110084, au kutembelea ofisi za Kanda zilizopo Dodoma,Dar es Salaam, Mwanza, Geita, Arusha, Mbeya, Mtwara na Tabora.”,Ilimalizia taarifa hiyo.