Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Ikoma, wakati walipotembelea Vituo vya uboreshaji katika Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Rorya mkoani Mara leo Novemba 27,2023.
Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira (kushoto) akizungumza jambo na Mwandishi Msaidizi katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Ikoma.
Mjumbe wa Tume, Mhe. Jaji Asina Omar akishuhudia BVR Operator, Felician Meena akiingiza taarifa za Mpiga Kura Mariam Wankyo aliyefika katika Kituo cha Kuandikisha Wapiga Kura cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji Ikoma kujiandikisha kuwa Mpiga Kura.
Mjumbe wa Tume, Mhe. Jaji Asina Omar akishuhudia BVR Operator, Felician Meena akimchukua alama za vidole Mariam Wankyo aliyefika katika Kituo cha Kuandikisha Wapiga Kura cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji Ikoma kujiandikisha kuwa Mpiga Kura.
Mpiga Kura Mariam Wankyo akionesha Kadi yake ya Mpiga Kura mara baada ya kukamilisha taratibu za Uandikishwaji.
Mpiga Kura akijaziwa taarifa zake.
BVR Opareta akichukua picha ya Mpiga Kura aliyefika kuandikishwa.
Mjumbe wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufaa Mwanaisha Kwariko akizungumza jambo na Mpiga Kura aliyefika kituoni kuboresha taarifa zake.
Mjumbe wa Tume, Magdalena Rwebangira akiangalia Mwandishi Msaidizi akimwandikisha Mpiga Kura.
Mwandishi wetu, Mara
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wameonesha kuridhishwa na zoezi la Uboreshaji
wa majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaoendelea katika
Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Mkoani Mara ambapo hadi kufikia
jana Wapiga Kura 1,613 wamejitokeza.
Wajumbe
hao wa Tume, Mhe. Jaji Asina Omar, Mhe. Jaji wa Rufaa Mwanaisha Kwariko na Mhe.
Magdalena Rwebangira wametembelea vituo vya uboreshaji katika Kata ya Ikoma na
kushuhudia ufanisi wa zoezi hilo.
Wakizungumza
wakati wa ziara hiyo, Jaji Asina Omar amesema mwitikio wa wananchi kujitokeza
kujiandikisha na kuboresha taarifa zao ni mkubwa na mawakala wanashiriki
kikamilifu katika zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuwabaini wananchi wasio na
sifa za kuandikishwa kuwa Wapiga Kura.
“Zoezi
linakwenda vizuri, tumeshuhudia katika vituo tulivyotembelea hakuna changamoto
na zilizopo zimetatuliwa na wataalam kwa kushirikiana na makawala wa vyama
waliopo vituoni jambo ambalo linaonesha lengo la zoezi hili kutimia kama ilivyo
kusudiwa,” alisema Mhe. Jaji Asina.
Jaji
Asina amesema, muda unaotumika kuandikisha au kuboresha taarifa za Mpiga Kura
unazidi kuwa mfupi na kuimarika kwa huduma vituoni hivyo kuleta ufanisi zaidi
siku hadi siku na kuonesha uwezo wa vifaa vinavyotumika.
Kwa
upande wake Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira
amesema ameridhishwa namna zoezi linavyofanyika hivyo lengo la zoezi hilo la
kufanyia majaribio vifaa vya uboreshaji pamoja na mifumo ya uboreshaji wa
Daftari linatimia kwani changamoto zinabainika na kutatuliwa mapema.
Akitoa
taarifa ya siku nne za uboreshaji huo wa majaribio katika Kata ya Ikoma,
Mkurugenzi wa Idaya ya Usimamizi wa Uchaguzi, Ndg. Grayson Orcado kwa niaba ya
Mkurugenzi wa Uchaguzi alisema, zoezi hilo linakwenbda vizuri na kwa ufanisi
mkubwa kwani hadi sasa wananchi 1,613 wamejitokeza vituoni ambapo kati ya hao 1,356 wamejiandikisha kuwa wapiga kura na wapiga kura 257 wameboresha taarifa zao huku
hakuna walioondolewa katika Daftari.
Orcado
amesema, mawakala wa vyama wanaonesha ushirikiano wa hali ya juu hasa katika
changamoto za utambuzi wa wakazi wa maeneo yao kwa kuzingatia kuwa Kata ya
Ikoma inamwingiliano wa raia wanchi jirani.
Kwa
mujibu wa mawakala wa vyama waliokuwepo katika kituo cha kujiandikisha wapiga
kura cha Shule ya Msingi Nyamasanda, walieleza kuwabaini raia 8 wakigeni kutoka
nchi jirani ambao walikiri kuwa si watanzania na hivyo Mwandishi Msaidizi
hakuweza kuwaandikisha kuwa wapiga kura.
Wakala
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Silvanus Owan’ge aliyepo katika
Kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata ya Ikoma amesema, wanarisdhishwa namna zoezi
hilo lilivyo la uwazi na kupongeza Tume kwa namna inavyofanya kazi kwa
kushirikiana nao.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
inaendesha zoezi la uboreshaji wa majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
katika Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara na Kata
ya Ng’ambo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoa wa Tabora kuanzia
tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.