OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema yuko tayari kutofautiana na Watumishi wachache watakaokuwa wanakwamisha utatuzi wa changamoto za Walimu ambao wanalitumikia Taifa hilo kwa Moyo.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo kwenye hafla ya kukabidhi Gari, Pikipiki 62 na Kompyuya mpakato 159 kwa Makatibu Wasaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu iliyofanyika kwenye shule ya Sekondari Tambaza mkoani Dar es salaam.
“Nikiwa Ofisi ya Rais – Utumishi chini ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita tuliwapandisha madaraja Walimu 227,363 na kuwabadilishia Walimu 11,642 lakini katika kufanikisha hili kuna Wakuu wa Idara ya Utumishi tuliwaondoa kwenye nafasi zao kwa sababu walikua wanakwamisha haki hizi za walimu.”
“Sasa nielekeze tena katika kipindi changu kusikia changamoto za Walimu kila mmoja wenye nafasi yake anayehusika kwa namna moja au kutatua changamoto za Walimu awajibike ipasavyo vingomevyo ntamchukulia hatua stahiki,”amesisitiza Mchengerwa
Amesema Kipindi hiki kitakuwa kigumu kidogo kwa wale wazembe katika kutekeleza majumuku yao lakini kitakua kizuri kwa wale wanaochapa kazi kwa maslahi ya watanzania.
“Nataka changamoto zote za walimu za kupandishwa madaraja na malimbikizo ya mishahara zikafanyiwe kazi ipasavyo,”amesema.
Awali, akizungumza katika Hafla hiyo Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Mwalimu Paulina Mkwama amesema vifaa hivyo vinavyokabidhiwa leo vitasaidia kuboresha utendaji kazi kwa Watendaji wa Tume na kuboresha utoaji wa huduma kwa Walimu.