*DG PSSSF
ateuliwa kuwa mtendaji bora 2023
*Wakurugenzi
wa Undeshaji, Fedha na TEHAMA, nao washinda
Na
Mwandishi Wetu, Dar
Kwa
mara ya pili mfululizo, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumishi wa Umma (PSSSF) CPA. Hosea Kashimba, ameibuka kidedea kwa kuwa
mshindi wa kwanza katika kundi la watendaji wakuu wa Taasis za Umma kwa mwaka
2023.
Mwaka jana, 2022 CPA. Kashimba
alijishindia tuzo hiyo pia. Kwa kushinda tuzo kwa mwaka huu, inaonesha wazi kuwa
Mkurugenzi Mkuu huyo wa Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) yupo makini katika utendaji wake.
Pamoja
na CPA. Kashimba, wakurugenzi wengine wa PSSSF wameongoza katika makundi yao.
Wakurugenzi
hao ni Mkurugenzi wa Fedha PSSSF, Bi.
Beatrice Musa-Lupi, ambaye ameshinda tuzo ya Mkurugenzi wa fedha wa mwaka, Bw. Mbaruku Magawa, ambaye amekuwa mshindi wa tuzo
ya Mkurugenzi Uendeshaji wa Mwaka na Bw. Gilbert Chawe, Mkurugenzi wa TEHAMA, ambaye yeye amekuwa miongoni mwa washindi wa tuzo ya Ubunifu na Teknolojia.
Tuzo
hizo za umahiri wa uongozi zinazotambulika kama The Top 100 Executive List 2023
Awards zimetolewa jijini Dar es
Salaam, mwishoni mwa wiki.
Akiongea
katika tafrija ya kukabidhi tuzo hizo, Mgeni Maalum Thamsanqa Maqubela, kutoka taasisi ya Global CEO Institute ya Jamhuri ya
Afrika Kusini; aliwaasa vingozi waliokabidhiwa tuzo kuendelea kuimarisha mbinu zao za kiuongozi
ili kuleta tija na ufanisi.
Aidha
aliwahakikishia kuwa Tanzania ina fursa nyingi za ukuaji wa haraka wa kiuchumi
na kwa kuzingatia fursa za kibiashara zilizopo sasa Afrika; basi matarajio ni
kuimarika kwa soko la hisa la Dar es Salaam (DSE).
Tuzo
hizi zinaratibiwa na waratibu wa Top 100 Executive Tanzania na Global CEO
Institute ya Jamhuri ya Afrika Kusini ili kutambua viongozi 100 mahiri kila
mwaka kwa kutathmini utendaji, umahiri, ustadi, ubora na uwezo.
hizi ni kielelezo cha umahiri na ukuaji wa taasisi katika kuonesha ukuaji wa
faida, ukuaji kifedha, ubunifu na huduma.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea
Kashimba (Kushoto), akipokea tuzo baada ya kuibuka mshindi wa kwanza “Tuzo za umahiri kwenye nyanja za
uongozi kundi la Hifadhi ya Jamii (The top CEO of the year – Parastatals
Category for year 2023), kutoka kwa mwakilishi wa Global CEO Institute ya
Jamhuri ya Afrika Kusin Thamsanqa Maqubela, katika hafla iliyofanyika mwishoni
mwa wiki jijini DSar es Salaa.
Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbaruku Magawa
(kushoto), akipokea tuzo ya “Mkurugenzi Uendeshaji wa Mwaka” wa Tuzo za Umahiri
kwenye nyanja za uongozi kundi la Hifadhi ya Jamii kutoka kwa Pastor Abraham
Essuman, kutoka Ghana. Tuzo hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam.
(kushoto), akipokea tuzo ya Ubunifu na Teknolojia katika hafla ya utoaji tuzo
za umahiri kwenye nyanja za uongozi kundi la Hifadhi ya Jamii kutoka kwa Bw. Yunus
Mwarabu, wa Ampola, Zanzibar. Tuzo hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) CPA. Hosea Kashimba (mwenye suti ya blue), akipongezwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Mbaruku Magawa (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Beatrice Musa-Lupi (kushoto) na Meneja wa PSSSF, Kanda ya Kinondoni, Bi. Ritha Ngalo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) CPA. Hosea Kashimba (wapili kushoto), akipongezwa na Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Gilbert Chawe (kulia), Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Mbaruku Magawa (wakwanza kushoto) na Meneja wa PSSSF, Kanda ya Kinondoni, Bi. Ritha Ngalo.