NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis,amewataka Watendaji wa Halmashauri za Wilaya,Mabaraza ya Miji na Manispaa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi ili kuepusha migogoro baina yao na Wafanyabiashara nchini.
Hayo ameyasema mara baada ya kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara wa Soko la Samaki katika Kijiji cha Konde katika ziara yake Kisiwani Pemba.
Mbeto,ametoa wito kwa Watendaji wa taasisi hizo kuhakikisha wanaendelea kufanya kazi zao kwa ueledi,juhudi sambamba na kutenda haki ili Wafanyabiashara walipe kodi na mapato kwa wakati na kukuza uchumi wa nchi.
Katika maelezo yake Mbeto, alisema Serikali inategemea mapato mbalimbali kutoka kwa Wananchi waliojiajiri katika Sekta ya biashara hivyo ni muhimu pande zote mbili kuendelea kushirikiana na kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria,kanuni na taratibu za nchi.
Alieleza kwamba wapo baadhi ya Watendaji wa taasisi za umma bado wanafanya kazi kwa mazoea,visasi na utashi binafsi na kuisababishia Serikali ukosefu wa kodi kwa makusudi na kwamba mtendaji yeyote atakayebainika Chama Cha Mapinduzi kitaishauri Serikali ichukue hatua za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma.
Aidha aliwasihi wafanyabishara kuendelea kufanya kazi zao kwa uadilifu na kuepuka makosa na migogoro hasa ya ukwepaji kodi halali za Serikali sambamba na kudumisha usafi wa mazingira katika biashara zao.
“Lengo la ziara yangu ni kusikiliza kero na changamoto zenu na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu, pia wito wangu kwenu endeleeni kulipa kodi na kufuata Sheria za nchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi ana imani kubwa kuwa Wafanyabishara ni kundi muhimu la kuendeleza maendeleo endelevu nchini’; alisema Katibu huyo Mbeto.
Akizungumza kwa niaba ya Wafanyabishara hao Ahmed Kassim Faki, alisema kuwa baadhi ya Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni wamekuwa wakiwakamata na kuwashitaki wafanyabiashara hao bila kutoa nafasi ya kujitetea na wengine kuchukuliwa bidhaa zao na kutozwa faini kubwa kuliko mitaji na vipato vyao.
Alifafanua kwamba kutokana na changamoto hizo kuna baadhi ya Wananchi wameshindwa kuendelea kufanya biashara hali inayoikosesha Serikali Mapato