Mkurugenzi wa Miradi Impacten Africa limited Bi.Winfrida Minja
Hermence Lullah Kaimu Meneja Idara ya Mahusiano Mgodi wa Barick Noth Mara
……………………
Impacten Africa Limited kwa kushirikiana na Mgodi wa Barick North Mara wametoa mafunzo kwa wajasiriamali ambao ni watoa huduma na wasambazaji wa bidhaa lengo likiwa kuwajengea Uwezo wa namna yakufanya kazi na Mgodi huo pamoja na namna bora ya kuwa walipaji wa Kodi Wazuri kwa serikali.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mkurugenzi wa Miradi kutoka Imapcten African Limited Bi.Winfrida Minja alisema mafunzo hayo endapo yatatumiwa vyema na wafanya Biashara hao yatasaidia kuongeza ukuaji wa Biashara zao pamoja na kutengeneza Ajira moja kwa moja kwa vijana ambao wamekuwa wakivamia Mgodi wa Barick kwa lengo la kuiba mapweq yanadhayodhaniwa kuwa na Dhahabu.
“Barick wamekuja na mafunzo hayo lengo nikuwajengea uelewa wenzetu wafanya biashara ambao wengine niwatoa huduma na wasambazaji wa bidhaa katika Mkoa huu wa mara natunaratarajia mafunzo haya yatakuwa na tija kubwa zaidi hasa kutoa ajira pamoja nakuwezesha wao pia kufanya biashara na kampuni ya Barick North Mara kwa kufata masharti kama walivyofundishwa”Alisema Winfrida Minja ambaye ni Mkurugenzi wa Miradi Kutoka Impacten Africa Limited.
Baadhi ya wafanya Biashara hao ambao wamenufaika na mafunzo hayo akiwemo Bwana Robert Marwa mkurugenzi wa kampuni ya RAEOA Investment amewashukuru Barick na Impacten Africa limited kuwawezesha katika Kupata Elimu hiyo kwani wanaimani sasa wafanyabiashara wa Mkoa wa Mara wataenda kuwa mabalozi Wazuri wa ulipaji Kodi nakufanya kazi ya usambazaji wa bidhaa katika Mgodi wa Barick North Mara kama mafunzo waliyoyapata kwa kuzingatia ubora wa bidhaa zao.
Akihitimisha mafunzo hayo Hermence Lulah Kazimi Meneja idara ya Mahusiano katika Mgodi wa Barick North Mara aliwataka wafanya biashara hao kwenda kuwa chachu ya mabadiliko katika uchumi pamoja na kuwainua vijana waliko katika maeneo yao kiuchumi badala ya kuwaza kuuvamia mgodini.
“Tuliagizwa na mkuu wa Mkoa wa Mara hasa kweny CSR kuhakikisha imatengwa fedha ambayo itasaidia kwa vijana kuhakikisha wananufaika na bado kuna Fedha nyingi ambayo inatarajiwa kutengwa karibu Bilioni 9 ambayo itaenda kwenye jamii kwa hiyo nawaomba muone Fursa na Nyinyi watoa huduma na wasambazaji wa bidhaa muone kwenye CSR kuna fursa”Alisema Hermence Lullah kaimu Meneja Idaya ya Mahusiano Mgodi wa Barick North Mara.