Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Damas Ndumbaro, Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Gerald Mongella amesema, lengo za mbio hizo ni kutangaza historia ya Kongwa hasa maeneo ya kihistoria yaliyotumiwa na Wanaharakati wa Ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika ikiwemo Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini, Namibia na Angola.
“Natumia nafasi hii kuangiza Kituo Cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika pamoja na Wilaya hii ya Kongwa, kuhakikisha mbio hizi zinakua endelevu, kuanzia mwakani (2024) washirikisheni Balozi za nchi zilizotumia eneo hili katika mafunzo ya kijeshi ili waweze kushiriki pamoja na wadau wengine ili mbio hizi ziwe za Kimataifa” amesema Mhe. Mongella.
Mhe. Mongella ameagiza Kituo hicho kiadhimishe Siku ya Afrika ambayo hufanyika kila tarehe 25 Mei katika Wilaya hiyo, ambayo imebeba historia kubwa ya Wanaharakati wa Ukombozi Afrika.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema amesema mbio hizo mbali na kuitangaza Kongwa lakini pia zimeibua fursa za Kiuchumi, ambapo amewaita wadau mbalimbali kuunga mkono mbio hizo kila zitakapokuwa zinafanyika.
Washindi katika mbio hizo wamepatiwa zawadi ya fedha taslimu pamoja na medali