Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Cde. Jokate Mwegelo akutana na kufanya mazungumzo na Baba Mwadhama Protace Kardinali Rugambwa.
Katika mazungumzo yao, Baba Kardinali amempongeza kwa kuaminiwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuchaguliwa na wajumbe wa kamati kuu kuwa Katibu Mkuu wa UWT Taifa.
Baba Mwadhama amemuahidi kumuweka katika Sala na anamkaribisha Kwa Ushauri Kila atakapohitaji katika kulitumikia Taifa la Tanzania.
Komredi Jokate Mwegelo amshukuru Baba Kardinali kwa mualiko na mapokezi mazuri, amuahidi ushirikiano na kuendelea kufanya vyema katika majukumu yake ya kuwaunganisha Wanawake, Vijana na Jamii nzima kwani amekuwa chachu kwa vijana wanaochipukia Kiuongozi na katika maswala mbalimbali yanayolenga kujenga jamii iliyobora na kuleta maendeleo endelevu Tanzania.
(Ninyi ni Nuru ya Ulimwengu,,, Nuru yenu iangaze watu wapate kuyaona Metendo Mema Yenu Mt. 5:14-15)