Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, leo amewasili mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Dkt. Biteko alipokewa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu.