Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzanua (JMAT) Tawi la Dar es Salaam, Mhe. Shabani Lila, amewahimiza Viongozi na wanachama tawi hilo, wakiwemo watumishi wengine wa mkoa huo, kujitokeza kwa ajili ya kuwatembelea na kutoa sadaka kwa watu wenye mahitaji maalum, katika tukio litakalofanyika Siku ya Jumapili ya tarehe 26 Novemba,. 2023.
Picha namba 1912 Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya matukio hayo, ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina alivitaja vitu vitakavyotolewa kwa wahitaji hao.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bi. Mary Shirima akiwa katika kikao hicho. Wengine ni wajume wa kikakao hicho.
……..
Na Magreth Kinabo- Mahakamas
Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzanua (JMAT) Tawi la Dar es Salaam, Mhe. Shabani Lila, amewahimiza Viongozi na wanachama tawi hilo, wakiwemo watumishi wengine wa mkoa huo, kujitokeza kwa ajili ya kuwatembelea na kutoa sadaka kwa watu wenye mahitaji maalum, katika tukio litakalofanyika Siku ya Jumapili ya tarehe 26 Novemba,. 2023.
Akizungumza katika kikao kilichofanyika tarehe 22 Novemba, 2023, kwenye ukumbi Namba Moja wa Mahakama ya Rufani Tanzania, uliopo jijini Dar es Salaam, Mhe. Jaji Lila, ambaye ni Mlezi wa tawi hilo, alisema matendo hayo ni ibada, hivyo wanachama wote na watumishi wanaalikwa ili kufanikisha tukio hilo.
Mhe. Jaji Lila, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tan zania, amesema katika matendo hayo watu wenye mahitaji maalum ambao ni watumishi wa Mahakama watapatiwa fedha kwa ajili ya kuwawezesha kuendelea kujikimu. Pia msaada wa vitu mbalimbali, hutatolewa kwenye Kituo cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu cha Mburahati ili kuwafanya wajisikie faraja.
“Katika tukio hili tutafanya kazi nao na kula chakula cha mchana pamoja ili kuwafanya wajisikie wako na walezi wao.” alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha Mhe. Lila amasema sehemu ya kukutana kwa ajili ya matendo hayo itakuwa ni eneo la Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Tanzania Dar es Salaam, kuanzia saa 3: 00 asubuhi, ambapo usafiri wa pamoja utakuwepo ili kuwawezesha watumishi kufika kwenye maeneo ya wahitaji hao kuanzia saa 4.00 asubuhi. Imehimizwa kwenye Kikao hicho, kila mshiriki kuwasili katika eneo la safari hiyo akiwa na hitaji lolote kwa ajili ya wahitaji. Kikao kiliazimia kuwa vazi la siku hiyo kuwa ni tisheti za JMAT aina yoyote ya Mahakama ya Tanzania.
Kwa upande wake, Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya matukio hayo, ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina alivitaja vitu vitakavyotolewa kwa watoto hao, kuwa ni michango ya vyumba vya kulala, magodoro, vyandarua,vitanda, mashuka, vikiwemo vitu mbalimbali vya matumizi ya nyumbani kama vile sabuni, mafuta, dawa za meno, nguo za aina mbalimbali.
Vitu vingine ni ada za shule na vyakula vya aina yoyote, taulo za kike na za watoto.