Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakati wa ziara yake katika wilaya ya hiyo akiwa kwenye ziara ya siku nne mkoani hapo. Naibu Waziri ameyasema hayo kufuatia malalamiko ya wa Umma kucheleweshewa malipo yao ya Likizo na stahiki nyenginezo.
Naibu Waziri ambaye yuko ziarani ameyasema hayo kufuatia vilio vya watumishi wa kada mbalimbali kuhusu malipo madogo kwa wachache wanapotaka kuomba likizo. Katika maelezo yake , ameeleza kuwa ili kuweza kupunguza vilio hivyo Halmashauri haina budo kuongeza makusanyo na hasa kuangazia vyanzo vipya vya mapato ili kutanua mtuko wa hazina ya halmashauri hiyo ikiwa pamoja na kuweza kulipa madai ya watumishi wake.
Halmashauri ya wilaya ya Iringa ni moja kati ya halmashauri zilizonyuma sana kimakusanyo hivyo kutegemea Ruzuku ya Serikali Kuu kujiendesha. Ushauri uliotolewa na Naibu Waziri ni wazi ukifanyiwa kazi halmashauri hiyo itaongeza makusanyo na hivyo kuweza kuhudumia watumishi wake huku serikali ikisaidia katika maeneo mengine.