Afisa Mawasiliano Mwandamizi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Semu Mwakyamjala akizungumza leo Novemba 23, 2023 katika maonesho ya wiki ya huduma za kifedha kitaifa yanayofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Afisa Mawasiliano Mwandamizi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Semu Mwakyamjala wakati alipokuwa akizungumza kwenye maonesho ya wiki ya huduma ya Fedha Jinini Arusha.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Semu Mwakyamjala akionesha machapisho yenye taarifa muhimu na maamdishi nundu kwa ajili ya watu wenye uoni hafifu.
……………………..
NA JOHN BUKUKU, ARUSHA.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa huduma ya mawasiliano nchini imeendelea kukua kutokana ongezeko kubwa la leseni kwa watoa huduma za mawasiliano ambazo zimefika 2,518.
Akizungumza leo Novemba 23, 2023 katika maonesho ya wiki ya huduma za kifedha kitaifa yanayofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Afisa Mawasiliano Mwandamizi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Semu Mwakyamjala, amesema kuwa wateja wa mawasiliano wamefikia 1,531, huku watoa za kuthibitisha ubora wa vifaa vya mawasiliano ni zaidi ya 2,000.
Bw. Mwakyamjala amesema kuwa ongezeko la watoa huduma imechangiwa kwa asilimia kubwa baada ya TCRA kuanza utoaji wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao inayojulikana kwa jina Tanzanite Portal.
“Muombaji anapaswa kuingia katika website ya TCRA ambayo ni www.tcra.go.tz na kuingia moja kwa moja na kujaza taarifa muhimu katika mfumo wa utoaji leseni na vyeti (Tanzanite Portal)” amesema Bw. Mwakyamjala.
Bw. Mwakyamjala amesema kuwa watu wote wanapaswa kutumia huduma hiyo kwa ajili ya kuomba leseni kwani ni fursa kwa watanzania kupata huduma bila kufika katika ofisi za TCRA.
Amesema kuwa utaratibu huo umewasaidia watu wengi kufanya maombi ya leseni bila kutumia gharama za kutumia nauli au kuandaa taarifa muhimu.
Amefafanua kuwa huduma zote za mawasiliano zitakuwa zinapatikana kwa njia ya mtandao ikiwemo kuomba, leseni, kufuta leseni pamoja na nyengine muhimu.
Katika hatua nyengine ameeleza kuwa TCRA imezindua klabu za kidigital kuanzia Shule za awali hadi vyuo vikuu kwa lengo la kuhamasisha masomo ya Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).
“Kuna kitabu cha muongozo wa klabu za kidigital katika Shule za awali hadi Vyuo vikuu ambacho kitawaongoza nini Cha kufanya ili kufikia malengo” amesema
“Lakini pia kipo kitabu chenye maamdishi nundu kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zetu wenye uoni hafifu ili wakati mafunzo yanatolewa kwenye hisi klabu za kidijital wasibaki nyuma waende pamoja na wenzao katika kupata ujuzi,”amesema Mwakyanjala.