Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mhandisi Jones Olotu akizungumza jambo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) leo Novemba 23, 2023 Jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Mbadala Jadidifu REA Mhandisi Aduera Mwijage akizungumza leo Novemba 23, 2023 Jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Daudi Kosuri akizungumza leo Novemba 23, 2023 Jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akizungumza leo Novemba 23, 2023 Jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakiwa katika Mkutano na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uliofanyika leo Novemba 23, 2023 Jijini Dar es Salaam ambao umeratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
……..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imejipanga kuhakikisha hadi kufikia mwezi June 2024 itakuwa imekamilisha utekelezaji wa kupelekea umeme katika vijijini vyote nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) leo Novemba 23, 2023 Jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mhandisi Jones Olotu, amesema kuwa utekelezaji wa kupeleka umeme unaendelea ili kufikia malengo tarajiwa.
Mhandisi Olotu amesema kuwa hadi kufikia june 2023 vijijini vyote vitakuwa vimefikiwa na umeme jambo ambalo litakauwa umemaliza utekelezaji kabla ya muda.
Amesema kuwa Tanzania bara kuna vijijini 12,313 na hadi kufikia sasa tayari wameunganisha umeme katika vijijini 11,313 huku vijiji 1,005 utekelezaji unaendeleaje.
“Lengo ni kuhakikisha tunawafikia watu wote katika kuhakikisha huduma ya umeme inapatikana katika vijijini vyote nchini” amesema Mhandisi Olotu.
Amebainisha wapo katika mipango ya kuvifikia vitongoji 36,101 ili viweze kupata huduma ya umeme huku akieleza kuwa hadi kufikia mwaka 2025 watakuwa wamefika malengo yao.
Amesema kuwa serikali kupitia REA imefanya utambuzi wa wigo wa mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji vyote Tanzania Bara ambavyo havijafikiwa na miundombinu ya umeme nchini.
Amesema kuwa gharama za kufikisha umeme katika vitongoji hivyo shilingi trilioni 6.7.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Daudi Kosuri, amesema kuwa vikao vya Wahariri na taasisi za umeme zinatoa fursa kwa watanzania kujua mafanikio ya serikali pamoja shughuli mbalimbali zinazofanywa ili kuleta tija.
Nae Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile ameupongeza utendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kufanya kazi kwa ufanisi huku akitoa wito wa kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na waandishi wa habari ili kuweza kufikia umma katika kutoa elimu katika nyanja mbalimbali.
Wakala wa Nishati Vijijini ulianzishwa kwa sheria ya nishati vijijini Na. 8 ya mwaka 2005 na kuanza kazi rasmi mwezi Oktoba 2007 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa iliyokuwa sera ya Taifa ya Nishati ya mwaka 2003.