Vailet Chiwango mhuhitimu wa shahada ya sayansi ya Usimamizi wa Rasilimali nyuki Kampasi ya Mizengo Pinda.
Amepata Tuzo ya mwanafunzi Bora wa jumla wa CHUO KIKUU CHA SOKOINE Cha KILIMO (SUA) katika sherehe za arobaini (40) za Tuzo
mwaka 2023.
Pia Vailet amepata Tuzo ya mwanafunzi Bora wa mwaka Kampasi ya Mizengo Pinda
Mbali na Tuzo hizo amepata Tuzo ya mwanafunzi Bora wa shahada ya Sayansi ya usimamizi wa Rasilimali nyuki mwaka wa tatu(03).
Ambapo Tuzo hiyohiyo pia imetolewa Kwa Ruth Peter msangi.
Kwa mwanafunzi Bora wa mwaka wa pili imeenda Kwa Nora Meck Mtikile ambaye anasoma stashahada ya Uzalishaji na Usimamizi wa Mazao
Wanafunzi wengine waliopata Tuzo Cosmas m. Cosmas ambaye anasoma shahada ya Sayansi ya usimamizi wa Rasilimali nyuki mwaka wa kwanza, Aloyse venance Kigwa stashahada ya Uzalishaji na Usimamizi wa Mazao mwaka wa kwanza, Salma Ramadhan Kigwangala mwaka wa pili shahada ya Sayansi ya usimamizi wa Rasilimali nyuki.
Mbali na Tuzo hizo zilitolewa Tuzo za Uongozi Bora katika serikali ya wanafunzi Suaso Tuzo ilienda Kwa Leha Naftar Josephat kama katibu mkuu mtendaji wa serikali ya wanafunzi, Upande kamishina wa Elimu na Mikopo imechukuliwa na Julius Elisha, Afya na Chakula na Mazingira Tuzo imeenda Kwa Mercy Magidanga na Tuzo ya usimamizi wa Mabweni Nelly Uswege Kwa wanawake na Upande wa wanaume Tuzo imeenda Kwa Victor Urio.