Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara akisisitiza jambo katika Kikao cha Maboresho ya Bandari (PIC) ya Dar es Salaam, kilichohusisha wadau wa Serikali, Taasisi na Sekta binafsi kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wadau wa Serikali, Taasisi na Sekta Binafsi wakifuatilia na kuchukua maelekezo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara (hayupo pichani) wakati wa Kikao cha Maboresho ya Bandari (PIC), kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
…………………….
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara amesema kuwa kuna umuhimu wa kuongeza nguvu katika utendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kushirikiana kwa karibu na wadau wa bandari ili kurahisisha mnyororo mzima wa Uchukuzi.
Akizungumza katika kikao cha Maboresho ya Bandari (PIC) kilichofanyika jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Prof. Kahyarara amesema kwa kushirikiana kwa karibu kutaongeza kasi ya upakuaji wa mizigo hasa katika kipindi hiki ambacho wadau wameanza kutumia mifumo ya tehama katika taratibu zote za kibandari.
“Taarifa iliyowasilishwa hapa inaonyesha ongezeko kuwa la kuhudumia meli nah ii imewezekana kupitia juhudi kubwa ambazo zimekuwa zikifanywa kwa kila mdau kufanya sehemu yake kwa ukamilifu,hivyo kuitia vikao hiiv tukiongeza nguvu zaidi meli zitaongezekan zaidi’” amesema Katibu Mkuu Prof. Kahyarara.
Prof. Kahyarara ametumia kikao hicho kuwapa taarifa wadau wote kuwa maboresho yanayoendelea kufanywa katika bandari hiyo yanatarajiwa kuongeza mzigo zaidi hivyo ni wakati muafaka kwa wadau kuweka mikakati madhubuti ya namna ya kuhakikisha huduma zinafanywa kwa wakati na kuhusisha wadau wote.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bandari wa Bandari ya Dar es Salaam Mrisho Mrisho amesema kuwa kwa mwezi Oktoba 2023 bandari hiyo imeweza kuhudumia Meli mia moja (100) na inatarajia kumaliza meli zilizotia nanga ili kuwezesha mizigo kuwafikia walaji kwa muda waliotarajia.
Naye mdau kutoka sekta binafsi Elius Lukumay amesema kwa sasa TPA ijielekeze kuzitangaza bandari za Tanga na Mtwara ili kuiwezesha kuunguza mzigo unaoelekea katika mikoa hiyo kuchukuliwa katika bandari ya Dar es Salaam.
Kikao cha Maboresho ya Bandari (PIC) hufanyika mara moja kwa mwezi ambapo hujumuisha Wizara za Viwanda na Biashara taasisi za Serikali ikiwemo Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Mamlaka ya Usafiri Ardhini Tanzania (LATRA), Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC), Wakala wa Misitu Nchini (TFS), Jeshi la Polisi na wadau wa sekta binafsi lengo likiwa kuhakikisha changamoto zinazoikabili bandari zinatafutiwa ufumbuzi kwa pamoja.