Na Sophia Kingimali
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile
Ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA) kuhakikisha wanasimamia miradi yao ili itekelezwe kwa muda uliopangwa.
Kauli hiyo ameitoa leo Novemba 22, 2023 jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo Lengo kubwa likiwa kufahamiana na kupata fursa ya kuonana na Menejimenti na kujionea shughuli zinazofanywa na mamlaka.
“Endeleeni kusimamia ubora wa miradi hiyo ili thamani ya fedha zilizotolewa mziwekee utaratibu mzuri wa kusimamia na maelekezo yaliyotolewa na viongozi yawe na mfumo ya utekelezaji,” amesema Kihenzile.
Amewataka pia TCAA waendelee kusimamia mashirika ya ndege ya ndani na nje ili kudhibiti ajali na malamiko ya wananchi ikiwa pamoja kuhairisha safari yaweze kutafutiwa ufumbuzi haraka.
Amesema kazi ya huku inataswira mbili moja inaenda sambamba kurekebisha na kujenga viwanja vya ndege sehemu mbalimbali TCAA wanasimamia ikiwemo Mtwara Arusha, Dodoma, Dar es Salaam na vinginevyo
“Zaidi ya mabilioni yameelekweza na bado Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatenga fedha ili kuhakikisha usalama wa vifaa vya mbalimbali vya angani ambavyo kimsingi vina dhibitiwa na vina simamiwa na TCAA,”amesema.
Aidha amesema ipo miradi kadhaa ambayo inafanyika mikubwa mojawapo ni ujenzi wa chuo cha usafiri wa anga ambacho kinafanya kazi kufundisha watu mbalimbali
“Tumeelezwa katika vyuo tisa Barani Afrika na TCAA ni kimojawapo na duniani vipo 35 tu Rais Dk Samia anapanga utaratibu wa kutenga fedha ili kuendelea kuwekeza zaidi kujenga chuo cha kisasa kama anavyofanya kwenye sekta nyingine”amesema
Kihenzile ameatoa wito kwa wafanyabiashara ndani na nje kuwekeza kwenye viwanja vya ndege nchini kwani usafiri wa anga nchini upo salama.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA),Hamza Johari amesema watahakikisha wanatekeleza maagizo yote yaliyotolewa kwa wakati.
“Naibu Waziri waAmetoa maelekezo ikiwemo katika suala zima la miradi kuhakikisha kwamba tunafanya miradi hiyo kwa viwango na ubora unaotakiwa na inamalizika kwa wakati,” amesema Johari.
Amesema mradi wa kubadilisha mifumo ya sauti ambayo wanaendelea nayo , kuboresha mawasiliano na mradi wa ujenzi wa chuo cha usafiri wa anga.
Amesema katika miradi hiyo yote mitatu watahakikisha maelekezo yatafanyiwa kazi kuwa miradi inafanyika kwa ubora na kumalizika kwa wakati kuwa viwango vya kimataifa.
Aidha ameongeza kuwa kuongezeka kwa mashirika ya ndege kutasaidia kupunguza gharama za nauli.