Na Sophia Kingimali
NAIBU Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye Mahafali ya 16 ya Chuo Cha Kodi (ITA) yatakayofanyika Novemba 24, 2023 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 22, 2023 jjini Dar es Salaam,Mkuu wa Chuo hicho Prof. Isaya Jairo amesema kuwa Wahitimu 508 kati yao Wanaume ni 293 na Wanawake 215 wanatarajiwa kuhitimu masomo yao kwa mwaka wa masomo 2022/ 2023 na Mahafali hayo yatafanyika Chuoni hapo.
Amesema kuwa Wahitimu watakao tunukiwa cheti cha Uwakala wa forodha na kodi ni 43, watakao tunukiwa stashahada ya Uwakala wa Usimamizi wa forodha na kodi ni 39, Watakaotunukiwa Stashahada ya juu ya forodha na kodi ni Wanne, Watakao tunukiwa Shahada ya forodha na Kodi ni 117, na wahitimu watakao tunukiwa Stashahada ya Uzamili ya kodi kwa mwaka huu ni 52.
Prof. Jairo, amesema kuwa Chuo Cha Kodi kinajivunia mafanikio mengi, lakini katika mpango mkuu wa tano wa chuo ambao umejikita katika kutoa mafunzo kwa njia ya kisasa ya Kidijitali.
Kwa kuzingatia uhusiano na ushirikiano wa Chuo Cha Kodi na Mamlaka za Usimamizi wa Kodi Afrika tayari Mamlaka ya Mapato Uganda wamethibtisha kuhudhuria Mahafali hayo.